Halmashauri ya Meru ina eneo la ukubwa wa kilometa za mraba zipatazo 1,268.2 na ki-utawala Halmashauri ya Wilaya ya Meru imegawanyika katika Tarafa 3 (Poli, Mbuguni, King’ori), Kata 26, Vijiji 90 na Vitongoji 337, Mamlaka moja ya Mji Mdogo wa Usa river, na Jimbo moja la Uchaguzi la Arumeru Mashariki.
Mamlaka ya Mji Mdogo wa Usa River ina Vitongoji 9. Mamlaka hii ilianzishwa tarehe 01 Januari 2009 kwa mujibu wa Kifungu cha 16 na cha 17 cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya mwaka 1982.
Halmashauri in jumla ya Madiwani 35, kati ya hao, Madiwani 26 ni wa kuchaguliwa na Madiwani 9 ni wa Viti Maalum.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa