Mratibu wa TASAF kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Boniface Mwilenga ameeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru imepokea fedha kiasi cha Milioni 188,651,580 kutoka TASAF makao makuu kwaajili ya zoezi la malipo kwa walengwa kwenye kaya 5485 wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF III) kutoka vijiji 47 kwa kipindi cha mwezi Mei/Juni 2018 ambapo katika fedha hizo Sh17,443,580 zitatumika kwaajili ya usimamizi ngazi ya wilaya na vijiji.
Mwilenga amesema lengo la Serikali kuwa na mradi huo wa TASAF ni kwaajili ya kuzinusuru kaya maskini kuwa na maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii hivyo amewaasa Walengwa wa TASAF III pindi watakapo pokea fedha hizo kutumia kwa malengo yaliyokusudiwa na mpango huo wa kunusuru kaya maskini.
Zoezi la uhuwilishaji wa fedha kwa walengwa kaya 5485 katika vijiji 47 litafanyika kuanzia tarehe 28 Mei 2018 hadi tarehe 1 Juni 2018 .
ORODHA YA VIJIJI 47 VYENYE WALENGWA WA TASAF III KAYA 5485
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa