Serikali kwa kutambua umuhimu wa mazoezi ya viungo kwakua mwili wa binadamu unahitaji mazoezi ili kuendelee kubaki katika hali ya afya nzuri ilitangaza kila jumamosi ya pili ya mwezi kua ni siku ya mazoezi ya viuono
kutofanya mazoezi ni hatari kwa afya na hakuna vidonge vya vitamini, dawa, chakula, au upasuaji unaoweza kuchukua mahali pa uhitaji wa kufanya mazoezi, ikumbukwe Mazoezi ya mara kwa mara au kufanya kazi zinazohusisha matumizi ya nguvu ya mwili yanasaidia mifumo mingi ya mwili kufanya kazi inavyotakiwa, mazoezi yatatuepusha na magonjwa mbalimbali kama magonjwa ya moyo,kisukari pia ni njia nzuri ya kupunguza uzito wa mwili uliozidi na hupunzisha akili.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya meru anawatangazia wananchi wote na watumishi wa serikali kua jumamosi ya tarehe 14 Octoba 2017 ni siku ya kufanya mazoezi ya viungo ,aidha anawatangazia kua mazoezi hayo yataanzia makao makuu ya Halmashauri kuelekea uwanja wa mpira Ngarasero Usa-River,wananchi wa maeneo ya mbali waafanye mazoezi hayo kwenye maeneo yao kwa faida za afya zao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa