Tarehe 25 Novemba hadi 10 Disemba kila mwaka Dunia inatekeleza kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa jinsia, Kwa Halmashauri ya Meru kupitia Idara ya maendeleo ya Jamii itaadhimisha siku hizi 16 za kupinga unyanyasaji na ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto tarehe 08 Disemba 2017 katika uwanja wa mpira Ngarasero Usa-River siku ya Ijumaa ya wiki hii ujumbe ukiwa “FUNGUKA, UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO HAUMWACHI MTU SALAMA.CHUKUA HATUA”
Aidha maazimisho haya yalianza tarehe 25/11/2014 na yatamalizika tarehe 10/12/2014 yakiwa na lengo la kupinga unyanyasaji wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii ngazi zote juu ya uwepo wa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa wananwake na Watoto ikiwa ni pamoja na kuimarisha harakati dhidi ya kupinga unyanyasaji huu na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Mgeni rasmi anatarajiwa kua Mkuu wa Wilaya ya Arumeru pia huduma ya upimaji wa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) itatolewa .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa