Ndg.Peter E. Kessy ambaye ni mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) aibuka mshindi wa uchaguzi mdogo Wa Diwani Kata ya King'ori uliofanyika leo .
Ushindi huo ni mara baada ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi Kata ya Kingori kumtangaza Peter Kessy kuwa mshindi kwa kupata idadi ya kura 4171 kati ya kura zilizopigwa 4220 sawa na asilimia 98 huku mpizani wake Ndg.George W. Nyambulye ambaye ni mgombea kupitia chama cha wananchi (CUF) kupata idadi ya kura 49 sawa na asilimia 1.2.
Aidha idadi ya kura zilizoharibika ni 18.
Msimamizi huyo wa uchaguzi Kata ya King'ori amesema uchaguzi huo umefanyika kwa amani na utulivu kwani wapiga kura wote waliofika kwenye vituo vya kupigia kura walipiga kura.
TEMBELEA TOVUTI www.merudc.go.tz.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa