Ndg.Bernald Kivundo ambaye ni mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) aibuka mshindi wa uchaguzi mdogo Wa Diwani Kata ya Majengo uliofanyika leo tarehe 13 Octoba 2018 .
Ushindi huo ni mara baada ya msimamizi wa uchaguzi Kata ya Majengo kumtangaza Bernald Kivundo kuwa mshindi kwa kupata idadi ya kura 1611 kati ya kura zilizopigwa 1690, huku mpizani wake Ndg. Naimani Nassary ambaye ni mgombea kupitia chama cha NCCR Mageuzi amepata idadi ya kura 70.
Aidha idadi ya kura zilizoharibika ni 09.
Msimamizi huyo wa uchaguzi Kata ya Majengo amesema uchaguzi huo umefanyika kwa amani na utulivu kwani wapiga kura wote waliofika kwenye vituo vya kupigia kura walipiga kura.
Ikumbukwe kuwa Kata ya Majengo ni miongoni mwa Kata 26 za Halmashauri ya Wilaya ya Meru katika Jimbo la uchaguzi Arumeru Mashariki.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa