Kutoka Jimbo la Arumeru Mashariki.
Ndg.Fanuel W. Nanyaro ambaye ni mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) aibuka mshindi wa uchaguzi mdogo Wa Diwani Kata ya Nkoanekoli uliofanyika leo tarehe 02 Disemba 2018 .
Ushindi huo ni mara baada ya msimamizi wa uchaguzi Kata ya Nkoanekoli kumtangaza Fanuel Nanyaro kuwa mshindi kwa kupata idadi ya kura 2303 sawa na asilimia 99.6 kati ya kura zilizopigwa 2313, huku mpizani wake Ndg. Hamisi Juma Kiemi ambaye ni mgombea kupitia chama cha CUF amepata idadi ya kura 04 sawa na asilimia 0.2.
Aidha idadi ya kura zilizoharibika ni 06.
Msimamizi huyo wa uchaguzi Kata Nkoanekoli amesema uchaguzi huo umefanyika kwa amani na utulivu na wapiga kura wamejitokeza kwa wingi sawa na asilimia 70.3 ya waliojiandikisha.
Ikumbukwe kuwa Kata ya Nkoanekoli ni miongoni mwa Kata 26 za Halmashauri ya Wilaya ya Meru katika Jimbo la uchaguzi Arumeru Mashariki.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa