Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru anawakaribisha wananchi wote, hususani vijana kwenye maadhimisho ya siku ya vijana kitaifa yatakayofanyika tarehe 12 Agosti 2018, katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Kata ya Akheri kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalumu Patandi Tengeru kuanzia saa 1:00 moja asubuhi.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Mhe.Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera,Bunge,Kazi,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu) .
Aidha maadhimisho hayo yataambatana na maonyesho ya wajasiriamali , burudani pamoja na upimaji wa magonjwa yasiyoambukizwa na ushauri juu ya mtindo bora wa maisha utatolewa.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya siku ya Vijana duniani 2018 "MAZINGIRA SALAMA KWA VIJANA"
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa