Halmashauri ya Wilaya ya Meru ni miongoni mwa Mamlaka za Serikali za mitaa zinazotekeleza mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF awamu ya III.
Mratibu wa TASAF kwenye Halmashauri hiyo Ndg.Boniface Mwilenga ameeleza kuwa Halmashauri hiyo imepokea fedha kiasi cha Milioni 194,947,580.00 kutoka TASAF makao makuu kwaajili ya zoezi la malipo kwa walengwa kwenye kaya 5485 wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF III) kutoka vijiji 47 kwa kipindi cha mwezi Julai/Agosti 2018 ambapo Kati ya kiasi hicho kiasi cha Tsh17,443,580 ni kwa ajili ya usimamizi ngazi ya vijiji, Kata na Halmashauri.
Aidha Tsh. 177,504,000 zitaalipwa kwa walengwa wa kaya maskini 5485.
Mwilenga amesema lengo la Serikali kuwa na mradi huo wa TASAF ni kwaajili ya kuzinusuru kaya maskini kuwa na maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii hivyo amewaasa Walengwa wa TASAF III pindi watakapo pokea fedha hizo kutumia kwa malengo yaliyokusudiwa na mpango huo wa kunusuru kaya maskini.
Zoezi la uhuwilishaji wa fedha kwa walengwa kaya 5485 katika vijiji 47 linaendelea
ORODHA YA VIJIJI 47 VYA WALENGWA WA KAYA 5485 WA (TASAF III)
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa