Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki anawatangazia wananchi wa Kata ya King'ori na Majengo kuwa kutakua na uchaguzi mdogo wa nafasi ya udiwani katika kata hizo utakao fanyika tarehe 13 Octoba 2018 siku ya Jumamosi ili kuziba nafasi wazi zilizoachwa na madiwani waliojiuzulu.
Aidha Msimamizi huyo wa uchaguzi ameeleza kuwa maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu hivyo vituo vya kupigaji kura vitafunguliwa kuanzia saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 kamili siku ya Jumamosi.
Wananchi wa kata husika ambao wamejiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura wanatakiwa kutumia haki yake ya msingi kwa kupiga kura ya kumchagua kiongozi anayemuhitaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa