Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru anawakumbusha wananchi wote kuwa Kesho Jumamosi tarehe 26 Mei 2018 ni siku ya Usafi wa Mazingira utakao fanyika kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi, ikikumbukwa kuwa Mhe. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alitangaza kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa ni siku ya Usafi wa Mazingira hivyo wananchi wote wafanye usafi kwenye maeneo yao .
Aidha kwa watumishi wa makao makuu ya Halmashauri wanatakiwa kufika saa 12:30 kwenye kituo cha afya Usa -River kwaajili ya kufanya usafi wa mazingira pia kwa watumishi wasio wa makao makuu wafanye usafi kwa kushirikiana na viongozi wa Kata na Vijiji.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa