Mkuu mkoa wa Arusha Mrisho Gambo anatarajia kufanya ziara ya siku moja kwenye Halmashauri ya Meru Wilayani Arumeru tarehe 27/09/2017, katika ziara hii yenye lengo la kujibu kero za wananchi ataambatana na uongozi wa Wilaya ya Arumeru na wataalamu wa Halmashauri hiyo ili kutoa ufafanuzi na majibu ya kero zitakazotolewa na wananchi.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa atazungumza na wananchi kwenye mikutano ya Hadhara katika eneo la Usa-River uwanja wa mpira Ngarasero majiraa ya saa tano asubuhi na mkutano mwingine utakua katika kata ya Malula kijiji cha Kolila majira ya saa saba mchana.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa