Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 20.09.2017 anatarajia kuanza ziara ya siku tatu mkoani Arusha. Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw.Mrisho Mashaka Gambo amesema baada ya kuwasili mkoani humo Rais Magufuli anatarajiwa kuzindua barabara ya KIA-Mererani inayoanzia Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) hadi mji wa Mererani mkoani Manyara yenye urefu wa kilometa 26.
Ifikapo Septemba 23, Rais Magufuli anatarajiwa kutunuku kamisheni kwa maafisa wa jeshi, tukio litakalofanyika katika uwanja wa Shekh Amri Abedi jijini Arusha.
Pia mkuu wa mkoa huyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuhudhuria sherehe hizo. Sherehe hizo ambazo kwa kawaida hufanyika katika chuo cha maafisa wa jeshi cha Tanzania Miliatary Academy (TMA) kilichopo Wilayani Monduli zitafanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja huo na hivyo kutoa fursa kwa wananchi wengi wa mkoa wa Arusha kushuhudia tuko hilo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa