Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ametoa wito kwa wazazi/walezi kuchangamkia fursa ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 ikiwa ni kampeni ya Siku 12.
Muro amesema hayo wakati wakati wa ufunguzi wa kampeni ya utoaji vyeti kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 katika Halmashauri ya Meru uliofanyika katika Hospitali ya Wilaya Tengeru.
Aidha,amesema cheti Cha kuzaliwa kinamanufaa makubwa kwani ni utambulisho rasmi wa Mtoto na takwimu za uandikishaji zitaisaidia Serekali kufanya mipango ,mikakati na uboreshaji wa huduma za watoto kama vile chanjo,miundombinu sekta ya Elimu nk."Serikali imewasogezea fursa ya vyeti vya kuzaliwa karibu, changamkieni fursa"amehimiza Muro
Muro amewataka Viongozi wa Serikali ,Madiwani, Watendaji wa Kata/ vijiji,Wenyeviti wa vijiji/Vitongoji na Maafisa Tarafa kuhamasisha na kuhakikisha watoto 40263 wa Halmashauri hiyo ambao ni wanalengwa wanaandikishwa.Pia, ametoa Rai kwa Viongozi wa Dini kuhamasisha jamii juu ya zoezi Hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Halmashauri ya Meru Mhe. Jeremia Kishili ametoa Wito kwa Madiwani wa Halmashauri hiyokutoa hamasa kwa jamii na wananchi ili wajitokeze kuwaandukisha watoto .
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt. Maneno Focus amesema Wananchi wameitikia zoezi Hilo ambapo kwa siku ya kwanza zaidi ya watoto 950 waliandikishwa.
Bi.Amina ambaye Miongoni mwa wazazi walioandikisha watoto ameishukuru Serikali kwa kusogeza huduma ya vyeti vya kuzaliwa kwa watoto ambayo vinapatikana ndani ya saa chache baada ya kujiandikisha.
IKumbukwe zoezi la utoaji vyeti kwa Watoto chini ya Miaka 5 lilianza rasmi tarehe 11 Mei 2021 katika vituo 79 zikiwa ni ofisi 26 za Kata na vituo 53 vya kutolea huduma za afya.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akikabidhi cheti kwa Mtoto Wakati wa Uzinduzi.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro Akizungumza wakati wa uzinduzi .
Bi.Amina akishuhudi binti take akikabidhiwa cheri acha kuzaliwa wakati wa uzinduzi.
Mganga Mkuu Wilaya Dkt.Maneno Focus akizungumza wakati wa ufunguzi.
Mhe.Jeremia Kishili Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa uzinduzi.
Baadhi ya wakati waliojitokeza wakati wa uzinduzi.
Picha ya pamoja ya Mratibu wa zoezi la utoaji vyeti Bi.Restuta Mvungi(gauni ya njano)wawezeshaji na maafisa waandikishaji wa zoezi la utoaji vyeti kwa watoto chini ya miaka 5.
Siku ya ufungaji mafunzo ya siku 3 kwa waandikishaji wasaidi
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa