Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango amekabidhi kwa Shule ya Sekondari Sing'isi
kompyuta mpakato 20 ikiwepo Kompyuta Kuu (server)yenye ukubwa wa GB 2000 ambayo imewekewa Vitabu vya ziada na kiada, mitihani ya Kitaifa ya masomo yote toka mwaka 1990 mpaka 2020 kwa ajili ya rejea kwa wanafunzi na walimu, video za masomo mbalimbali ikiwa ni Sehemu ya Kompyuta 580 zilizotolewa na wadau wa Reneal international Education Outreach Wilayani humo.
Ruyango ametoa wito kwa wadau kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuongeza wigo wa matumizi sahihi ya TEHAMA katika Shule za Msingi na Sekondari na kuutaka Uongozi wa Shule ya Sekondari Sing'isi kuhakikisha Kompyuta hizo zinatunzwa na kuhifadhiwa vyema Ili kuwa na tija iliyokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya ametoa wito kwa Walimu kutimiza wajibu wao kwani mwalimu ana nafasi Kubwa ya kumjengea Mwanafunzi msingi thabiti wa kielimu,pia niwakati wa Walimu kujiendeleza katika masomo ya ICT "tuwajengee misingi ya kesho yao" amehimiza Mwl.Makwinya
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sing'isi Mwl.Datus Muganga amesema walimu na Wanafunzi watanufaika na Kompyuta hizo, kwani zinarahisisha ufundishaji na wanafunzi wanapata fursa ya kujisomea na kufanya majaribio mbalimbali .
Afisa TEHAMA Mkoa wa Arusha Ndg.David Nyangaka amesema programu ya utoaji wa Kompyuta kwa Shule za Serikali inayofanywa na shirika la Reneal international Education Outreach imezaa matunda Mkoani humo kwani baadhi ya Halmashauri wanafunzi wamefanya mitihani ya kitaifa ya ICT na matokeo yanaridhisha.
Diwani wa Kata ya Sing'isi Mhe.Elisa Nassari amesema Kata hiyo itaendelea kuhamasisha wadau kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akiwasili katika Shule ya Sekondari Sing'isi pamoja na viongozi alioambatana nao.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Akikabidhi kompyuta kwa mmoja wa Walimu wa Shule ya Sekondari Sing'isi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Sing'isi.
Mkuu wa Shule ya Sing'isi Mwl.Datus Muganga akishukuru baada ya kukabidhiwa Kompyuta .
Afisa TEHAMA Mkoa wa Arusha Ndg.David Nyangaka akizungumza wakati wa kukabidhi kompyuta kwa Shule ya Sekondari Sing'isi
Diwani wa Kata ya Sing'isi Mhe.Elisa Nassari akizungumza Katika Shule ya Sekondari Sing'isi
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Sing'isi.
Walimu wa Shule ya Sekondari Sing'isi
Walimu Shule ya Sekondari Sing'isi
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa