Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Meru Boniface Mwilenga ametoa rai kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini katika Halmashauri hiyo kufanya matumizi sahihi ya fedha wanazopokea ili kuleta tija kwakuboresha hali ya maisha yao.
AidhaMwilenga amefafanua kuwa kila baada ya miezi miwili Serikali kupitia mfukowa TASAF imekua ikitenga fedha kwaajili ya malipo kwa walengwa 5,485 kutoka vijiji 47 katika Halmashauri hiyo.
AidhaHalmashauri ya Wilaya ya Meru ilipokea shilingi 188,051,580.00 kutokaTASAF makao makuu kwa ajili ya Malipo na Usimamizi wa malipo hayo kwa walengwa5,485 wa Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF III) katika vijiji 47 kwakipindi cha mwezi Semtemba/Octoba 2018.
Jumlaya shilingi 170,608,000.00 zitalipwa kwa walengwa ,kiasi cha Tsh.4,700,000ni kwaajili ya usimamizi wa malipo kuanzia ngazi ya kijiji.na kiasi 12,038,580ni kwaajili ya malipo ngazi ya Halmashauri.
Zoezila malipo kwa walengwa limeanza tarehe 04 Octoba 2018 na litakamilika tarehe 10Octoba 2018.
TASAF "pamoja tuondoe umaskini"
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa