• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU YATUMIA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 308 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 HADI KUFIKIA MWEZI APRILI 15, 2020

Imewekwa: April 19th, 2020

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ndg. Emmanuel Mkongo amesema Halmashauri hiyo katika kuunga mkono jitihada za wananchi kutekeleza miradi  ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 ilitenga kutoka katika makusanyo ya mapato ya ndani jumla ya shilingi milioni 515 na kutumia shilingi milioni 308 katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ununuzi wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba 21 vya madarasa na vyumba 3 vya maabara sambamba na ununuzi wa viti na meza ikiwa ni mkakati wa Halmashauri hiyo kuendelea kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu kwa kukamilisha vyumba vya madarasa na maabara ili kutatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi kutokana na ufaulu mkubwa wa wanafunzi walioingia kidato cha kwanza mwaka huu na mkakati wa kuboresha ufundishaji wa masomo ya Sayansi.

Aidha , Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya milioni 18,961,020.06 kwa Shule ya Sekondari Maroroni na Sing'isi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara, Mkongo amesema vifaa hivyo vimegawanywa kwenye Kata zote 26 kwa kutoa kipaumbele kwa Kata ambazo Wananchi wake wameonesha juhudi za kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo  akitolea mfano Kata ya Maroroni na Sing'isi na kutoa wito kwa wananchi wa Kata nyingine kufanya vizuri zaidi.

Aidha, Mkongo ameongeza  fedha hizo  jumla ya Shilingi milioni 308 za Mapato ya Ndani ya Halmashauri na  Shilingi Milioni 50,666,300 za mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo ambao Mwenyekiti wa Kamati ya ya Mfuko huo ni Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki  Dkt. Danielson Pallangyo zimechochea kwa kiasi kikubwa ujenzi na ukamilishaji wa Miundombinu hiyo.

 Aidha, Mtendaji wa Kata ya Maroroni Bi. Lyidia Sarakikya amemshukuru Mbunge Dkt.Pallangyo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kutoa mbao, bati na mifuko ya saruji kwaajili ya kukamilisha vyumba 3 vya madarasa kwani imewatia wananchi moyo kwa kupunguza  ukali wa michango.

Naye Mkuu wa Shule ya sekondari Maroroni Mwl. Felix Nibigira ameishukuru Serikali na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa wazazi kutokubweteka kipindi ambacho shule zimefungwa badala yake wawasimamie wanafunzi kufanya mazoezi yaliyotolewa kwani shule hiyo iliwaandalia majaribio na masomo kwa kifurushi kilichopewa jina la HOME PACKAGE.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ndg. Emmanuel Mkongo


Mtendaji wa Kata ya Maroroni Bi. Lyidia Sarakikya akizungumza baada ya kupokea vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya milioni 11, 209,770.02

Mtendaji wa Kata ya maroroni wakati wa kukabidhiwa bati kwaajili ya kukamilisha vyumba vya madarasa .

Mwonekano wa Vyumba 2 vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Maroroni iliyopokea vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 11  ikiwa ni mifuko ya saruji 50,mbao  zenye thamani ya milioni 6,201,000  na bati  110


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa