Wananachi wa Kata ya Uwiro na Ngabobo waunga mkono matumizi ya Uzazi wa mpango ili kutoa malezi bora kwa watoto na kuboresha Afya ya Mama ,hili limedhihirishwa na wawakilishi toka kata hizo ambao ni wenyeviti wa Vijiji, wajumbe wa Serikali za vijiji, viongozi wa kimila, viongozi wa kiroho, wakunga wa jadi, viongozi wa vijana na kinamama na baadhi ya Wanachi , baada ya kupata semina juu ya matumizi ya mpango wa uzazi na umuhimu wa mama mjamzito ambaye mimba itaharibika kusafishiwa hospitali pamoja na umuhimu wa kujifungulia Hospitali, kwenye Semina ya Matumizi ya uzazi wa mpango iliyotelewa imetolewa na wahudumu wa afya wa jamiii waliopewa mafunzo na shirika la Engender Health ambao ni Elizabeth Richard na Piterson N. Nnko iliyofanyikia katika Kituo cha Afya cha Ngarenanyuki tarehe 13 Disemba 2017.
Aidha wawakilishi hao wamepongeza uwepo wa semina hiyo iliyofadhiliwa na Shirika la Engender Health kwa kushirikia na Halmashauri ya Meru na kutoamsimamo kua wataelimisha na kuwahamasisha wananchi wengine ambao hawajapata fursa hii ya kuhudhuria semina hiyo kutumia njia za uzazi wa mpango, sambamba wanawake wajawazito kujifungulia kwenye Hospitali (vituo vya Afya) pamoja na wajawazito ambao mimba zitaharibika kuhakikisha wanapata huduma ya kusafishwa kizazi kwenye Hospitali.
Martha Yakobo ambaye ni Mkunga wa Jadi amesema baada ya kupata elimu kupitia semina hiyo kwa sasa atakua mstari wa mbele kuhamasisha kina mama wajawazito kujifungulia Hospitalini kwa usalama wao na usalama wa mtoto atakayezaliwa pia atawashauri wanawake kutumia uzazi wa mpango ili kuboresha malezi kwa watoto na Afya ya mama.
Salome J. Mbegela ambaye ni Mratibu wa Uzazi wa mpango kwenye Halmashauri ya Meru ameitaka jamii hiyo kuondokana na mtizamo hasi kuhusu matumizi ya uzazi wa mpango kwani hauna madhara yoyote kwani yeye binafsi ameutumia kwa zaidi ya miaka 20 pia ametoa elimu juu ya njia zote za uzazi wa mpango na kueleza umuhimu wa kutumia vituo vyaa afya kupata huduma mbalimbali ikiwemo kujifungua.
Salome J. Mbegela ambaye ni Mratibu wa Uzazi wa mpango kwenye Halmashauri ya Meru akieleza umuhimu na faida za kutumia uzazi wa mpango
Sebastian A. Macrice ambaye ni mratibu wa shirika la Engender Health akihimiza mama mjamzito anapoharibikiwa na mimba kuhakikisha anasafishwa kizazi kwenye Hospitali(kituo cha Afya)
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa