Kampeni ya jiongeze tuwavushe Salama imezinduliwa katika Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru ambapo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Mhe.Jerry Muro, amesema Wilaya hiyo itasimamia vyema Kampeni hiyo inayolenga kupunguza vifo vya mama wajawazito pamoja na watoto wachanga, hivyo jamii na watoa huduma za afya wanapaswa kutekeleza wajibu wao kwa wakati "kuwa mjamzito na kujifungua si ugonjwa hivyo kinamama na watoto ni lazima wawe salama kwani uhai ni haki yao"amesisitiza Mhe Muro.
Aidha Muro amemwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus Kuwakumbusha watoa huduma za afya kutekeleza wajibu wao kwa weledi pia kutumia lugha zenye staa na rafiki kwa wagonjwa sambamba na kuacha matumizi ya simu za mkononi yasio muhimu wakati wa saa za kazi "kauli nzuri kwa mgonjwa humpa faraja na kuwa sehemu ya tiba" amefafanu Muro.
Mganga Mkuu Dkt.Maneno Focus amesema Serikali imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuhakikisha dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma vinakuwepo ambapo kwa Halmashauri hiyo hali ya uwepo wa dawa muhimu wakati wa kujifungua ni zaidi ya asilimia 98.
Aidha Dkt. Focus aliainisha kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka 2019 kumekua na vifo viwili vitokanavyo na uzazi ingawa bado kuna changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi toka kwenye jamii ambao hawafiki kwenye vituo vya kutolea huduma, hivyo kampeni hiyo inalenga kuongeza uwajibikaji kwa viongozi wa dini, siasa, kijamii na wadau wote kuwajibika na kuhakikisha vifo vya uzazi vinadhibitiwa.
Naye Mratibu wa Kampeni hiyo ngazi ya Halmashauri Ndg.Sikudhani Mkama amesema Halmashauri imeweka mikakati ya kuhakikisha utekelezaji wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama inafanikiwa na ametoa rai kwa jamii na familia kutimiza wajibu wao ili kupunguza na kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi.
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Afya Philomena Marijan toka Shirika la kimataifa lisilo laSerikali DSW ambalo huwawezesha vijana kwa kuwajengea mazingira wezeshi pamoja na kuongeza ushiriki wao katika ma swala ya afya ya uzazi,uchumi na uongozi, ameipongeza Halmashauri hiyo kulipa kipau mbele swala la afya ya vijana na elimu juu ya afya ya uzazi.
Aidha uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri umekamilika kwa maafisa Tarafa kula kiapo cha usimamizi wa utekeleza wa Kampeni hiyo.
PICHA ZA TUKIO
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze tuwavushe Salama.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt.Maneno Focus.
Kiongozi wa Mila ,Mzee wilson Kaaya,Mshili mkuu ukoo wa Kaaya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe Salama.
Philomena Marijani toka Shirika la kimataifa lisilo laSerikali DSW akizungimza kwa niaba ya wadau wa afya.
Picha ya pamohja Meza kuu na wadau wa Afya.
Mhe.Diwani kata ya Akheri (wa kwanza kulia) Viongozi wa Dini na Mila wakati wa uzinduzi.
Watumishi wa Idara ya Afya wakati wa uzinduzi .
Wakuu wa idara Halnashauri ya Meru wakati wa uzinduzi
Wadau wa Afya
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa