• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Mahusiano mazuri kwa Waalimu yatajwa kuinua Taaluma.

Imewekwa: March 1st, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro ametoa wito kwa  Maafisa elimu Sekondari,Wakuu  wa shule za sekondari na Maafisa elimu Kata pamoja na walimu kufanya kazi kwa ushirikiano kufikia malengo ya Serikali ya kutoa elimu bora kwa kila mtoto wa kitanzania.

Muro ametoa wito huo wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha tathimini ya matokeo ya mtihani wa Taifa  kuhitimu kidato cha nne na mtihani wa upimaji kidato cha pili katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kilicho wajumusisha Wakuu  wa Shule 68 za Serikali na binafsi, Maafisa Elimu wa Kata  26 .

Aidha, Muro ameitaka Idara ya Elimu Sekondari na Wakuu wa Shule kuhakikisha wanafanyia kazi maazimio ya Kikao hicho ikiwa ni  pamoja na kudhibiti utoro shuleni na kazini ili kuendelea kufanya vizuri kwenye Taaluma katika Halmashauri hiyo inayoshikilia nafasi ya 3 ya kitaifa katika matokeo ya kuhitimu kidato cha Nne mwaka 2020.

Afisa Elimu wa Halmashauri hiyo,  Mwl .Emmy Mfuru amesema asilimia ya ufaulu katika Mtihani huo wa kuhitimu kidato cha Nne imepanda   kutoka 90.8 mwaka  2019 hadi  94.5 mwaka 2020 .

Mfuru amepongeza  jitihada za Walimu katika ufundishaji zilizopelelea Halmashauri hiyo kutetea nafasi ya 3 kitaifa kwa miaka 2 mfululizo katika matokeo ya kuhitimu kidato cha nne na kuahidi kufanya ufuatiliaji wa maazimio ya kikao hicho.

Ndg.Emmanuel Mkongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amewapongeza walimu wa shule zilizo fanya vizuri na kusisitiza umuhimu wa walimu kushirikiana "Ushirikiano ni sehemu ya mafanikio , mwalimu akiwa na amani na utulivu atafanya kazi yake kwa bidii na ufanisi mkubwa"amesisitiza Mkongo.

Mkongo ametoa wito kwa Walimu kuwa mstari wa mbele kuwasaidia wanafunzi kupenda na kusoma masomo ya Sayansi kwa kuwajengea uelewa wa umuhimu wa kusoma masomo hayo na faida baada ya kuhitimu "Ilani ya Uchaguzi inasisitiza kuwa na Elimu inayojikita katika  Sayansi na Teknolojia kwa kuhakikisha Wanafunzi wanapata stadi na maarifa ya  kujitegemea kulingana na Mazingira ya Nchi yetu. Aidha, Sera ya Nchi yetu ni kujenga Uchumi wa Viwanda ambao  umejikita kwenye Sayansi na teknolojia" amefafanua Mkongo.

Kikao kazi hicho kimehitimishwa katika ukumbi wa Halmashauri hiyo huku kikiwa na maazimio ya  kupandisha hali ya ufaulu, kukomesha utoro shuleni, ufuatiliaji wa ufundishaji, ushirikiano baina ya shule moja na nyingine .


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akizungumza kwenye kikao cha tathimini ya matokea ya mtihani wa Taifa  kuhitimu kidato cha nne na mtihani wa upimaji kidato cha pili katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru .

Ndg.Emmanuel Mkongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru  akizungumza wakati wa kikao.

Afisa Elimu wa Halmashauri hiyo,  Mwl.Emmy Mfuru akizungumza wakati wa kikao.


Katibu tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Mchembe ametoa wito kwa walimu kuwa wazalendo katika  uwajibikaji

Afisa taaluma idara ya sekondari Mwl.Abdnego Mulokozi akisoma taarifa ya hali ya ufaulu matokeo  ya kidato cha nne.Kushoto ni Afisa taaluma Mwl.Neema  Mbio.

Walimu wakuu  wa shule za sekondari wakati wa kikao.

Walimu wakuu  wa shule za sekondari wakati wa kikao.

Walimu wakuu  wa shule za sekondari wakati wa kikao.

Walimu wakuu  wa shule za sekondari wakati wa kikao.

Walimu wakuu  wa shule za sekondari wakati wa kikao.

Walimu wakuu  wa shule za sekondari wakati wa kikao.

Walimu wakuu  wa shule za sekondari wakati wa kikao.

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa