Kampeni ya NILINDE MIMI NA MAMA YANGU TUISHI inayolenga kuzuia vifo vya mama na watoto wachanga imezinduliwa Mkoani Arusha wakati wa kikao cha kujadili vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Elimu maalumu Patandi ,kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru..
Akizindua kampeni hiyo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa,amesema kampeni hiyo ni miongoni mwa mikakati ya Mkoa wa Arusha kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga.
Aidha, Muro ametoa wito kwa wahudumu wa afya,watendaji wote wa Serikali na jamilii kutekeleza wajibu wao na kushirikiana ili kuhakikisha wanapunguza au kumaliza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga "hatutegemei kuwa na vifo vya mama au watoto ambavyo vimesababisha na uzembe''amesisitiza Muro.
Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Wedson Sichalwe amesema kikao hicho ni kwa mujibu wa matakwa ya kisera ambapo hufanyika kila robo ya mwaka kikilenga kupunguza kasi ya vifo hivyo , japo takwimu zinaonesha mafanikio ya kupungua kwa vifo ambapo mwaka 2019 kulikuwa na vifo 67 na mwaka 2020 vilipungua kufikia 46 bado jitihada mahsusi zinahitajika.
Ndg.Emmanuel Mkongo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amesema kunaumuhimu mkubwa kutoa elimu kwa jamii juu ya dalili hatarishi kwani jamii ina kipaumbele kupunguza vifo kwa kuwawahisha wajawazito kuwahi hospitali,kuhudhuria cliniki pamoja na kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Mkongo amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri hiyo kupitia mapato yake ya ndani itajenga kituo cha afya katika Kata ya Maroroni kitakacho gharimu Shilingi Milioni 400 ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuzuia vifo vya wajawazito na watoto wachanga.
Kikao hicho kilichojumuisha timu za usimamizi wa afya ngazi ya Mkoa ,Wilaya na viongozi wa Halmashauri ya Meru kinatarajiwa kuendelea kwa siku nne ikiwa ni pamoja na wajumbe kufanya usimamizi shirikishi katika halmashauri ya Meru.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza .
Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Wedson Sichalwe akizungumza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa