Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg.Charles Kabeho amefungua Miradi miwili daraja la Irikolanumbe na mradi wa barabara ya Ubungo Irikolanumbe yenye thamani ya Shillingi 338,490,000 .
Aidha Ndg.Kabeho ameridhishwa na ujenzi wa mradi wa daraja la Irikolanumbe ambalo limekidhi vigezo tofauti na barabara ya Ubungo -Irikolanumbe yenye urefu wa km 2.9 ambayo ilionekana kuwa na mapungufu kinyume na mkataba
Baada ya kubaini mapungufu hayo Ndg.Kabeho ameagiza mkandarasi aliyefanya kazi hiyo kutolipwa hadi atakaporekebisha mapungufu hayo ,pia ametoa angalizo kwa Taasisi za umma kutofanya kazi na wakandarasi wasumbufu "hakuna haja ya kufanya kazi na wakandarasi wasumbufu kama huyu wanarudisha maendeleo nyuma" amesisitiza Ndg.Kabeho.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe.Jerry Muro amesema atafanyia kazi maagizo ya kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ndani ya siku zisizozidi saba.
Mradi wa daraja la irikolanumbe na Barabara ya Ubungo - Irikolanumbe ni miongoni mwa miradi ya Halmashauri ya Meru iliyopitiwana mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akikagua barabara ya Ubungo - Irikolanumbe.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akipima upana wa barabara ya Ubungo - Irikolanumbe.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akisubiri kuona mkataba na hatua za maandishi alizochukuliwa mkandarasi anayetengeneza barabara ya Ubungo - Irikolanumbe.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akitoa maelekezo baada ya kukagua barabara ya Ubungo - Irikolanumbe na kupitia mkataba.
Wananchi wa Kata ya Nkoarimbu -Ndoombo wakisubiri ufunguzi wa Miradi miwili daraja la Irikolanumbe na mradi wa barabara ya Ubungo Irikolanumbe.
Mradi wa daraja la Irikolanumbe kabla ya ufunguzi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg.Charles Kabeho akiweka jiwe la ufunguzi wa daraja la Irikolanumbe na mradi wa barabara ya Ubungo Irikolanumbe
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa