Serikali yatatua changamoto ya maji katika Shule ya Sekondari Kisimiri iliyopo Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru inayoshikilia rekodi ya nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu kidato cha sita mwaka huu .
Akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo, Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais TAMISEMI Gerald Mweli amepongeza Uongozi wa Wilaya, Halmashauri, Walimu na Wanafunzi kwa matokeo mazuri ya kidato cha sita sambamba na matokeo ya kidato cha nne mwaka huu ambapo wanafunzi 99 walipata ufaulu wa daraja la kwanza (division one).
Mweli ameeleza kuwa Serikali imetoa shilingi milioni 60 za uchimbaji kisima kirefu cha maji shuleni hapo ili kuondoa changamoto hiyo iliyotajwa kuwa kikwazo kikubwa kwa walimu na wanafunzi.
Mweli ametoa rai kwa wanafunzi kuendelea kufanya vizuri zaidi na kuwa wazalendo "Somo la historia ya Nchi yetu litafundishwa kwa kiswahili mmebahatika kuwa wakwanza kujifunza historia ya Nchi yenu.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia Dkt. Leonard Akwilapo amepongeza jitihada za Mkoa wa Arusha katika sekta ya Elimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, ameishukuru Serikali kwa mradi huo wa uchimbaji wa kisima kirefu ambao utelelezaji umeshaanza kwa kuwashirikisha Wakala wa Serikali wa Uchimbaji Visima na Mabwawa ambao upo chini ya Usimamizi wa RUWASA.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi wameishukuru Serikali kwa kutatua changamoto ya maji na kuomba kutatuliwa kwa changamoto ya umeme ambao umekua ukiwaka kwa baadhi ya maeneo ya shule.
Awali, Makatibu Wakuu hao walitembelea Shule ya Sekondari ya Mfano Nchini ya Patandi Maalum iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambayo imeanza rasmi tarehe 22.02.2021.
aibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais TAMISEMI Gerald Mweli akizungumza na wanafunziwa Shule ya sekondari Kisimiri.
Wanafunzi wa Shule ya Kisimiri wakati wa Ziara ya Makatibu Wakuu.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisimiri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Emmanuel Mkongo akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisimiri.
Mkuu wa shule ya kisimiri Mwl. Valentine Tarimo.
Walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri wakati wa Ziara ya Makatibu Wakuu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa