Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru Timotheo Mzava amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha milioni 500 kwa ajili ya uboreshaji wa kituo cha Afya cha Usa-River kwa lengo la kusogeza huduma karibu na Wananchi pia kuviboresha vituo vya Afya kuwa na hadhi ya vituo vya Afya.
Mzava amesema fedha hizo zitatumika kujenga miundombinu kwenye kituo hicho cha Afya ikiwa ni ujenzi wa jengo la upasuaji, wodi ya mama na mtoto, maabara, jengo la kuhifadhia maiti, nyumba ya mtumishi, Jengo la utawala ,kichomea taka pamoja na ukarabati wa majengo yaliyopo, pia amewataka wananchi kushiriki kuchangia ujenzi huu ikiwa ni pamoja na nguvu kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kilichopo kituo hicho cha Afya Christopher J. Kazeri ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha hizo kiasi cha Milioni 500 kwa ajili ya uboreshaji wa Kituo cha Afya Usa-River kwani kwenye Bajeti ya Halmashauri hiyo haikwepo, pia amewasihi wananchi kuitikia wito na kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano kwa kuzingatia muda .
Wananchi waliohudhuria mkutano huo wamesema wapo tayari kushiriki na kumiliki mradi huo wa uboreshaji wa kituo cha Afya ikiwa ni baada ya kuzingatia ushauri uliotolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru wa kuchagua wawakilishi 10 wanaotakiwa, ambao ni waadilifu, waaminifu, wakweli na wenye moyo wa kufanya kazi hiyo ya kujitolea. Pia wananchi hao wameishukuru Serikali kwa kuwezesha uboreshaji wa kituo hicho cha Afya
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt. Cosmas Kilasara amewasihi wananchi kumiliki kituo hicho cha Afya Usa-River kwa kukitumia pamoja na kulinda miundominu ya kituo hicho.
Daktari msimamizi wa kituo hicho cha Afya Usa-River Elinasi E. Nyari amesema kituo hicho kitakapo kamalika kitaweza kuwahudumia watu Zaidi ya 13,320, hivyo itapunguza msongamano kwenye Hospitali za Wilaya na Mkoa, pamoja na kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto
Wawakilishi wa wananchi wa Kata yaUsa-River kutoka vitongoji vyote vinavyounda Kata hiyo watakao shiriki kwenye uboreshaji wa kituo cha Afya Usa-River
(wa kwanza kulia) ni Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Timotheo Mzava,katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru ,Christopher J. Kazeri na wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Meru Cosmas Kilasara waki jadiliana jambo wakiti wa mkutano wa wananchi wa Kata ya Usa-River.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa