Walengwa wa mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Halmashauri ya Meru,Wilayani Arumeru wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuweka akiba na kutunza kumbukumbu kwa vikundi kutoka Kijiji cha Ngurudoto na Ngyeku, wameishukuru Serikali kwa kuwatoa katika hali duni ya maisha kupitia malipo ya ruzuku ya fedha kila mwezi toka mwaka 2015 hadi sasa ambapo wanaweza kupata mahitaji muhimu kama chakula ,mavazi ,kusomesha watoto na wengi wao wameweza kuanzisha miradi ya ufugaji ,kilimo,biashara ndogo ndogo pamoja na kujenga nyumba.
Walengwa hao wamesema mafunzo hayo yaliyotolewa kwa siku mbili jana na leo, yalikuwa muhimu kwani wameshapewa vitendea kazi ambavyo ni nyaraka mbalimbali na sanduku la kuhifadhia fedha hivyo walikua hawajapata uwelewa wa kina ambao utawasaidia kuendesha vikundi ,kuweka kumbukumbu,taratibu za kukopa na uwekaji akiba.
Christina Mbise ambaye ni mlengwa na mwanakikundi wa kikundi cha Agape amesema TASAF imekuwa mkombozi kwake kwani mbali na kuwa maskini na kuingizwa kwenye TASAF akiwa mjane kwa kipindi cha miaka hii 3 aliweza kutumia ruzuku ya fedha anazolipwa na TASAF kwa matibabu madogo dogo ya mtoto wake ambaye ni mlemavu wa ubongo pia waliweza kupata mahitaji ya chakula na mavazi.
Christina amesema hakuishia kutumia ruzuku hizo kwa mahitaji madogo bali alijiingiza kwenye shughuli za kiuchumi kwa kufuga mbuzi na badae alimuuza akahamia kwenye kukuza vifaranga vya kuku ambavyo baada ya kukua aliviuza na kupata faida ya sh.400,000 ambapo aliamua kutumia kiasi cha fedha hizo kumpeleka mwanae mlemamu shule ya ufundi na kiasi kingine anajishughulisha na biashara ndogondogo.
Christina amewaomba wadau wa maendeleo kumsaidia mwanae huyo ili apate matibabu zaidi na makazi kwani mara nyingi huanguka na kuzimia hivyo kuwa kero kwa majirina wengine katika nyumba ya kupanga anayoishi."nilijitahidi nikanunua kiwanja kidogo lakini nimegundua kipo kwenye mkondo wa maji"ameeleza Christina
Aidha Mafunzo hayo ya kuvijengea uwezo wa kuweka akiba na kutunza kumbukumbu kwa vikundi vya walengwa wa TASAF yalianza kwa kuwajengea uwezo wa kuvifundisha vikundi wawesheshaji ngazi ya wilaya kwa siku 3 tarehe tarehe 25,26,27 Juni 2019 ambapo kwa sasa wataendelea kutoa mafunzo kwa vikundi vyote vya walengwa wa TASAF vilivyobaki ikiwa mafunzo kwa Vikundi 7 Kijiji cha Ngyeku na Vikundi 11 katika Kijiji cha cha Ngurudoto yamekamilika.
Ikumbukwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru yenye Vijiji 90 ,Vijiji 47 vipo katika mpango wa kunusuru kaya maskini ,na Vijiji 20 katika Vijiji hivi 47 vina jumla ya vikundi 122 vyenye wanachama 1732 kati yao wanawake ni 1544 na wanaume 188,vinatarajiwa kupewa mafunzo haya.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya ,Mwl.Julius Myovela akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Amani katika Kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya ,Antipas Massae akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Upendo Kati katika Kijiji cha Ngurudoto.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya ,Ndg.Geturde Mkubwa akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Mwema katika Kijiji cha Ngurdoto.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Sheila Mrogoro akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Umoja katika Kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya ,Ndg.Florence Saria akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Agape Kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Spora Mtali akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi chakatika Kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Donata Minde akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Upendo katika Kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Elipokea Nassary akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Tumaini katika Kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Fatuma Kafuku akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Faraja katika Kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya ,Ndg. Mariana Mkiramwene akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Baraka katika Kijiji cha Ngyeku.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Anna Nduguru akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Betheli katika Kijiji cha Ngurdoto.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Lea Leina akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Amani katika Kijiji cha Ngurudoto.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya clementina Mbise (mwenye sweta jeusi)na Esta Mbwana (sweta jeupe ) wakitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha katika Kijiji cha Ngurudoto.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Mary Kiondo akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Amani katika Kijiji cha Ngurdoto.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Joyce Mruge akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Neema katika Kijiji cha Ngurudoto.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Digna Masawe akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Ndenigwa katika Kijiji cha Ngurdoto..
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Eunice Obed(mwenye sweta nyeusi) akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Upendo katika Kijiji cha Ngurdoto.
Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Agnesi Mbiseakitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu kwa wanakikundi cha Tumaini katika Kijiji cha Ngurudoto.
Kiongozi wa wawezeshaji wa TASAF Ngazi ya Taifa Ndg.Hosea Mwankusye akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo katika kijiji cha Ngyeku,wa kwanza kulia kwake ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ngyeku Ndg.Elibariki Mungure, na wa pili Kulia kwake
Mfatiliaji wa TASAF Halmashauri ya Meru Judith Masika Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara baada ya mafunzo katika kijiji cha Ngyeku.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Meru ,Ndg.Boniface Mwilenga baada ya mafunzo katika kijiji cha Ngyeku
mwezeshaji wa TASAF ngazi ya taifa Hamza Seleman kwenye mkutano wa hadhara baada ya mafunzo katika kijiji cha Ngurudoto.
Christina Mbise ambaye ni mlengwa na mwanakikundi wa kikundi cha Agape akishuhudia namna TASAF ilivyombadilishia maisha.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa