Wito watolewa kwa maafisa waandikishaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka 5 kuwa waadilifu wakati wa zoezi Hilo litakalo anza tarehe 11 MEI 2021 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Dkt.Maneno Focus ambaye amwemwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, amewataka waandikishaji wasaidizi hao kufuatilia kwa makini mafunzo hayo yatakayo wawezesha kutekeleza zoezi la uandikishaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 kwa ufasaha kama ilivyokusudiwa.
Aidha , Dkt.Focus ametoa Wito kwa waandikishaji hao kuwa waadilifu na kuwajibika wakati wa uandikishaji "zoezi hili ni nyeti linahitaji UADILIFU mkubwa"amehimiza Dkt.Focus.Halmashauri ya Wilaya ya Meru imejiwekea lengo la kuwafikia watoto 31,400 wenye umri chini ya miaka 5 ambao hawana vyeti vya kuzaliwa.
Dkt.Focus amehitimisha kwa kutoa wito kwa wazazi wenye watoto chini ya miaka mitano ambao hawana vyeti vya kuzaliwa kufika ofisi za Kata na vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia siku ya Jumatatu ya tarehe 11 Mei ili kutengenezewa vyeti bila gharama yote.
Restuta Mvungi ambaye ni mratibu wa zoezi Hilo amesema wazazi watatakiwa kufika kwenye vituo vya uandikishaji vilivyopo katika Kata zote 26 za Halmashauri hiyo wakiwa natangazo la kizazi au Kadi ya Kliniki ikiwa na jina la mtoto na majina matatu ya wazazi wote wawili au cheti Cha ubatizo nk.
Amefafanua kuwa zoezi Hilo litadhumu kwa muda wa Siku 12 za kampeni uandikishaji Kuanzia tarehe 11 hadi 22 Mei 2021 na baada ya hapo litakuwa endelevu.
Aidha zoezi la uandikishaji watoto wenye umri chini ya miaka 5 katika Halmashauri ya Meru litafanyiwa katika ofisi za Watendaji wa Kata 26 za Halmashauriya Wilaya ya Meru pamoja na vituovya kutokea huduma za afya.
Ikumbukwe zoezi hilo litafanyika katika Mkoa wa Arusha na Manyara likitoa fursa kwa watoto kutambulika .
Dkt.Maneno Focus alizungumzia wakati wa mafunzo.
Bi.Restituta Mvungi akizungumza wakati wa mafunzo
Waandikishaji Wasaidizi wakati wa mafunzo
Waandikishaji Wasaidizi wakati wa mafunzo
Waandikishaji Wasaidizi wakati wa mafunzo
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa