Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru,Mch. Anael Nassari wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wilaya la Ushirika lililofanyika katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Wilaya ya Meru amemkabidhi mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Jerry Muro Shuka 30 kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa kwenye vituo vya Afya.
Mchungaji Nassari ameeleza kuwa Vyama vya Ushirika mbali na kuwajengea uwezo wa kujikomboa kiuchumi pia kati ya misingi saba ya Ushirika,mmojawapo ni kuijali jamii hivyo kuna baadhi ya Vyama vilishatoa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa shule lakini kupitia Jukwaa hilo wameshiriki kuboresha huduma za afya kwa kujitolea shuka hizo.
Akipokea mchango wa shuka hizo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amepongeza juhudi za Ushirika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma za Afya ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa kwa asilimia 100% kwenye wilaya hiyo.
Mhe. Muro amesema serikali ya awamu ya tano inahakikisha wananchi wake wanapata huduma bora za afya ampapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 wilaya hiyo imepewa bilioni moja na Milioni 400 kwa ajili ya kuboresha vituo vya Afya vitatu, Usa – River, Nduruma na Mbuyuni .
Mh. Jerry Muro amekabidhi shuka hizo kwa Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Cosmas Kilasara kwa ajili ya matumizi katika kituo cha Afya Usa-River.
Kituo cha Afya Usa-River Kilichopo Halmashauri ya Meru kiliboreshwa kwa milioni 500 huku vituo vya Afya viwili Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ambavyo ni Nduruma kuboreshwa kwa milioni 500 na Kituo cha Afya Mbuyuni mwishoni mwa mwaka wa fedha 2017/2018 kimepokea milioni 400 na uboreshaaji unaendelea.
Uboreshaji wa Vituo vya Afya hufanyika kwa ujenzi wa majengo ya kisasa ya wodi ya mama na mtoto, upasuaji, maabara ,nyumba za watumishi pamoja na vyumba vya kuhifadhia maiti pia kukarabati majengo yaliyopo.
Uundaji wa Majukwaa ya ushirika ngazi ya Mkoa na Wilaya hutoa fursa kwa Vyama vya Ushirika kukutana kubadilishana mawazo, kupeana uzoefu, kujadili changamoto zinazoukabili Ushirika na kuweka mikakati ya kutatua changamoto hizo.
PICHA ZA TUKIO.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro na Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Wilayani Arumeru Mch.E Nassari wakati wa makabithiano ya shuka kwaajili ya vituo vya Afya.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Cosmas Kilasara akipokea shuka toka Mkuu wa Wilaya ya Arumeru .
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akiwashukuru wanaushirika kwa kuungamkono Uboreshaji wa Huduma za Afya Wilayani hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirika Halmashauri ya Meru Mkumbwa Mussa (kulia ) pembeni yake ni Afisa ushirika kwenye Halmashauri ya Meru Neema Mundo.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa