• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

WATAFITI WA KISAYANSI NAFASI YA PILI KITAIFA WATOKA SHULE YA SEKONDARI KISIMIRI.

Imewekwa: August 19th, 2019

Shule ya Sekondari Kisimiri iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilaya ya Arumeru , ambayo ilishika nafasi ya kwanza Kitaifa katika matokeo ya kidato cha Sita mwaka 2019, imeendelea kufanya vizuri Kitaifa ambapo wanafunzi wake wa tafiti za kisayansi wameshika nafasi ya pili Kitaifa katika mashindano ya Kitaifa ya Vijana watafiti wa kisayansi  yaliyofanyika Jijini Dar es salaam tarehe  tarehe 01 - 02 Agosti 2019,

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisimiri Mwl.Valentine Tarimo mbele ya Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wakati Kamati hiyo ilipofika shuleni hapo kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Aidha Mwl.Valentine  amefafanua  kuwa katika mashindano hayo yaliyoshirikisha Shule 97 zenye wanafunzi 194, Wanafunzi wanne (4) kutoka Shule ya Sekondari Kisimiri walishiriki na kuibuka washindi  wa  pili huku nafasi ya kwanza ikienda kwa wanafunzi toka Shule ya Sekondari Chief Dodo iliyopo Mkoa wa Manyara na nafasi ya tatu ilichukuliwa na wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari St. Jude ambayo pia ipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.


Ushindi huo  ulipelekea Shule ya Sekondari Kisimiri kushika nafasi ya pili na kutunikiwa tuzo tatu, pia wanafunzi walioshiriki walipewa medali na fedha kiasi cha sh.1,500,000 .

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amepongeza juhudi za walimu, wanafunzi na wazazi katika kuinua kiwango cha elimu katika Shule ya Sekondari Kisimiri na kuhaidi kutoa ushirikiano kwa shule hiyo ili iendelee kufanya vizuri zaidi.

Aidha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango imekamilisha ziara yake kwa  siku ya kwanza kwa kukagua miradi ya Ujenzi wa nyumba ya mtumishi (Mganga) katika zahanati ya kijiji cha Ngabobo, Ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Ilikirimuni, Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Shishtoni na  Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Ngejusosia Kata ya Malula.  

Wanafunzi Joseph  Masangu na Vicent Gabriel Laizer  walioshinda tuzo ya mshindi wa pili Kitaifa.

Wanafunzi Albert  Muhagama and Enid Nobert walishinda tuzo Maalumu.

Wanafunzi 4 walioshiriki Mashindano wakiwa na walimu wao.

(wa pili kutoka kushoto)Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaua ya Meru Mhe.Will Njau,kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti Nelson Mafie,kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Kisimiri Mwl.Valentine Tarimo ,Wa pili kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Emmanue Mkongo kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu ,afya na mazingira Elisa  Mungure wakifurahia tuzo za ushindi.

Picha ya pamoja ya Kamati ya Fedha utawala na mipango , Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisimiri .


Mkuu  wa Shule ya Sekondari Kisimiri akitoa maelezo kuhusu mradi wa ujezi wa nyumba za walimu 6i in one.


Ujezi wa Mradi wa Zahanati ya kijiji cha Ngabobo.

Mhe.Diwani Kata ya Ngabobo Solomon Laizer akitoa ufafanuzi juu ya ujenzi wa Mradi wa Zahanati ya Kijiji cha Ngabobo.

Ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Ilikirumuni Kata ya Ngarenanyuki.

Mtendaji wa Kijiji cha Elikirimuni Akisoma taarifa ya ujezi wa Mradi wa Zahanatiya kijiji hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meruwakati wa ukaguzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ilikirimuni.

Mwenueki wa Halmashauri akipata maelezo toka kwa mtaalamu wa Idara ya ujenzi.

Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Shishiton Kata ya Maruvango.

Wajumbe wa Kamati ya fedha ,mipango na utawala wakisomewa taarifa ya ujenzi wa kijiji cha Shishiton toka kwa Mtendaji wa Kijiji hicho.

Ujenzi wa Zahanati ua kijiji cha Ngejisosia Kata ya Malula.

Wajumbe wa Kamati ya fedha,utawala na Mipango wakikagu ujenzi wa Zahanati ya kijiji chaNgejisosia.

Diwani Kata ya Malula,ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri akitoa ufafanuzi juu ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ngejososia.

Wajumbe wa kamati ya fedha,utawala na mipango wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Mradi wa Zahanati kijiji cha Ngejisosia.



Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa