• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

NAIBU WAZIRI WA MAJI MHE.AWESO ASIMAMISHA ZIARA YAKE KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI.

Imewekwa: August 24th, 2019

Naibu Waziri wa maji Mh. Juma Aweso amelazimika kusimamisha ziara yake  kwa muda mfupi kusikiliza  kero za wananchi wa Kijiji cha Oldonyongiro Wilayani Arumeru kuhusiana na maji ili hali kuna mradi wa maji wa MAKILENGA  unaohudumia vijiji 22 kikiwemo kijiji hicho.

Wakitoa malalamiko yao juu ya upatikanaji wa maji Kijijini hapo wananchi hao wamelaani kitendo cha kufungiwa maji na wananchi wenzao wa ukanda wa juu ambapo ndipo mradi unapo anzia ilihali wapo tayari kuchangia gharama za maji.”Kinamama tunateseka tunatumia muda mwingi kufuata maji  kwa sababu ya kubaguliwa kwa kufungiwa Maji na watu wa Kata ya Leguruki  wanaotumia maji ya bomba kumwagilia”alisema Mwaija Omari.

Mwananchi mwingine alijitambulisha kwa jina la  Matayo, amesema uongozi wa bodi ya Maji MAKILENGA  umekua ni kikwazo kwani badala ya kutatua changamoto wameendelea kupewa maji kwa mgao ambapo wanaweza  kukosa huduma ya maji kwa zaidi ya siku 3.  

Aidha Mh. Aweso aliwaomba wananchi hao    kuwa wavumilivu na kuendelea na ziara yake inayolenga kutambua na kutatua changamoto za upatikanaji maji kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayo elekeza ifikapo mwaka  2025 upatikanaji maji vijijini kuwa asilimia 85.

 Kufuatia malakamiko hayo Naibu huyo  ameagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Arumeru kuwashikilia na kuwaweka chini ya ulinzi viongozi wa Bodi hiyo akiwemo mwenyekiti wa Bodi Godhope Chales,Mhasibu wa Mradi Bi.Warialanga Pallangyo,pamoja na fundi bomba anayetambulika kwa jina la Kaaya, kwa tuhuma za ubadhirifu”Serikali haitamfumbia macho yeyote atakaye fanya ubadhirifu wa miradi ya maji na imejikita kuwaletea wananchi maendeleo”amesisitiza Aweso.

Aweso amesema kwa mujibu wa Sheria no 5 ya mwaka 2019 iliyoanzisha mamlaka ya maji vijijini na Mjini RUWASA vyombo vya vya watumia  maji ikiwemo MAKILENGA vitaundwa upya hivyo hii itaboresha uongozi pia ameagiza uundaji wa tume itakayochunguza uendeshaji wa mradi huo wa MAKILENGA.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Jerry Muro amesema  hakuna tatizo la Maji Kijijini hapo bali tatizo lipo kwa Wananchi wenyewe  na uongozi wa MAKILENGA kwani miradi ya maji iliyopo inauwezo wa kuhudumia vijiji vyote 22 vilivyopo kwenye Mradi hivyo ameshauri  wenyeviti wa Vijiji vyote 22  kuwa wajumbe wa bodi  ili waweze kusimamia  upatikanaji wa maji kwenye vijiji vyao.


Kwa upande wake Meneja wa Wakala  wa Maji  Vijijini Wialaya ya Arumeru  mhandisi Christine Kessy amesema kwa mujibu wa Sheria  ya Maji no 12 ya mwaka 2009 inaelekeza kuwa, Maji ni rasilimali ya taifa  na yanatakiwa yalindwe hivyo hakuna mwananchi anayeruhusiwa kuzuia upatikanaji wa huduma ya Maji pia Sera ya maji ya mwaka 2002 inaelekeza  nilazima kwa wananchi wote kuchangia. 

                           

Mhandisi Christine ameeleza  kuwa Wananchi wa Kata ya Leguruki  wamechangia mradi huo kutokufanya vizuri kwani wanatumia maji ya bomba hovyo  kumwagilia migomba na kahawa pia  hawachangii huduma ya maji.

Ziara ya Mhe.Naibu Waziri wa Maji imekamilika kwa kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, ambapo Mhe.Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki DKt.John Pallangyo amewashukuru wananchi kwa kumchagua na kuahidi kuwatumikia  na kuwawakilisha vyema .


Mhe.Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki John Pallangyo akizungumza na Wananchi wa Tarafa ya King'ori.

Mhe.Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki John Pallangyo amewashukuru wananchi hao kwa kumchagua na amehaidi kuwatumikia na kuwawakilisha vyema.pia amewaomba ushirikiano.

ananchi wakimsikiliza Mhe.Mbunge.

Wananchi wakimsikiliza Mhe.Mbunge.



Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE SEMINA YA MAFUNZO YA UCHAGUZI MKUU 2025 October 16, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • DED MERU DC AKABIDHI VYETI KWA TAASISI ZINAZO FANYA VIZURI MERU DC

    August 07, 2025
  • TFS YATOA MSAADA WA MBAO TAKRIBANI MIA 8 HOSPITALI YA WILAYA YA MERU

    August 07, 2025
  • MERU DC YAIBUKA MSHINDI WA PILI MAONYESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI

    August 08, 2025
  • UZINDUZI WA JENGO LA TEHAMA SHULE YA SEKONDARI PATANDI MAALUM

    August 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa