Timu ya uendeshaji huduma za afya (CHMT) Halmashauri ya Wilaya ya Meru, yagawa kadi za mfuko wa afya wa jamii ulioboreshwa (ICHF) kwa watoto 105 wenye mahitaji maalumu katika shule ya Msingi patandi maalum iliyopo katika Halmashauri hiyo
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus amesema timu hiyo imewakatia bima hizo wanafunzi kama sehemu ya upendo kwa , kuboresha mahusiano na jamii sambamba na kuhamasisha jamii kujiunga na bima ya ICHF ili kuweza kupata matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa gharama yaelfu 30 tu.
Maneno amesema timu hiyo ya kwa kutambua umuhimu wa matibabu wakati wote inahamasisha Kaya elfu 58 ambazo hazitumii bima yoyote kujiunga na ICHF ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu muda wote kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa gharama ya shilingi elfu 30.
Mratibu wa ICHF Wilaya Ndg.Adalbet Temba amesema bima ya ICHF yenye gharama ya shilingi elfu 30 inatumika kulipia gharama za huduma zote za msingi ikiwa ni kumwona daktari,dawa na vipimo vya msingi ambapo ametoa wito kwa jamii kujiunga na bima hiyo .
Temba amesema mwananchi anaweza kujiunga na ICHF kwa kufika ofisi ya mtendaji wa kijiji ili kuunganishwa na afisa mwandikishaji ambapo atapaswa kulipa shilingi elfu 30 ikiwa ni bima kwa wanakaya 6 yaanimkuu wa kaya mwenza na wategemezi 4 ambao watapata huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati ,Kituo cha afya,Hospitali ya Wilaya na hospitali za rufaa .
Temba amehitimisha kwa kufafanua kuwa bima ya ICHF itatumika kwakuzingatia rufaa, yani mwanachi atapaswa kutibiwa kuanzia ngazi ya Zahanati,Kituo cha afya,Hospitali ya Wilaya na hospitali ya rufaa ya Mkoa .
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mwl.Marcus Nazi, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi amepongeza timu ya CHMT Pia ametoa wito kwa wazazi wenye wanafunzi katika shule za msingi na sekondari kuungana kuwakatiawanafunzi hao bima za ICHF ili kuwa nauhakika wa matibabu wakati wowote“Wanafunzi 5 wanaweza kupata bima ya ICHF kwa kipindi cha mwaka mmoja kwagharama ya shilingi elfu 30 tu “amesisitiza Mwalimu Nazi.
Mwl. Jackline Mtui ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Patandi maalum ameishukuru kamati ya CHMT kwa kuwakatia wanafunzi 105 wenye ulemavu shuleni hapo ambao wanachangamoto ya akili,Usonji,wasioona na viziwi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mwl.Marcus Nazi, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi bima za ICHF kwa Wanafunzi105 wenye mahitaji maalum.
Mganga Mkuu wa Halmashaurhi hiyo Dkt.Maneno Focus akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi bima za ICHF kwa Wanafunzi105 wenye mahitaji maalum.
Mratibu wa ICHF Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Adalbet Temba akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi bima za ICHF kwa Wanafunzi105 wenye mahitaji maalum.
Mwl.Jackline Mtui ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Patandi maalum akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi bima za ICHF kwa Wanafunzi105 wenye mahitaji maalum.
Wanafunzi wa SHule ya Msingi Patandi maalum walionufaika na bima za ICHF
Mwl. Marcus Nazi akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kadi ya ICHF zilizotolewa na timu ya HMCT Halmashauri ya Meru.
Naomi ni miongoni mwa wanafunzi 105 wanufaika wa bima za afya ICHF zilizotolewa na timu ya HMCT Halmashauri ya Meru.
Miongoni mwa Wanufaika wa bima za afya ICHF zilizotolewa na timu ya HMCT Halmashauri ya Meru.
Mkuu wa shule ya Msingi Patandi Maalum Mwl. Jackline Mtui akipokea zawadi za wanafunzi toka kwa mgeni rasmi.
Picha ya pamoja ya Meza kuu na Wanafunzi wa shule ya Msingi Patandi maalumu.
Wajumbe wa kamati ya HMCT Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa hafla ya kukabidhi bima za ICHF kwa wanafunzi 105
Picha ya pamoja mgeni rasmi,Walimu wa shule ya patandi Maalum na timu ya HMCT Wilaya.
Wajumbe wa kamati ya HMCT Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Wajumbe wa kamati ya HMCT Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Wajumbe wa kamati ya HMCT Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa