Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru imetoa wito kwa wananchi wa Wilaya hiyo kuwasilisha hoja na kero zao kwa kufuata utaratibu unaokubalika ikiwa ni kuziwasilisha ofisi za Vijiji, Kata, Halmashauri na ofisi ya Mkuu wa Wilaya .
Hayo yamejiri baada ya mwananchi mmoja kunukuliwa akikwamisha shughuli za ujenzi wa barabara ya Ndoombo - Sanks chini ya TARURA, ambapo aliwazuia wataalam kuendelea na shughuli sambamba na kutumia lugha isiyo na staa iliyopelekea Ofisi ya Mku wa Wilaya kumtaka kuripoti kwa Mkuu wa kituo cha polisi Wilaya ya Usa-River ili utaratibu wa kisheria uchukue mkondo wake.
Aidha, ofisi hiyo haitaweza kumvumilia mwananchi yeyote atakaye zuia maendeleo na kufanya jambo lolote kinyume cha Sheria.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa