Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Jonathan Kiama anawatangazia wananchi wote wenye umri wa kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea, kujiandikisha kwenye Orodha ya Wapiga Kura kuanzia leo tarehe 08 - 14/2019.
Nenda ukajiandikishe kwenye Kituo kilivyoainishwa kwenye Kitongoji chako.
Tumia vizuri muda uliopangwa, hakikisha umejiandikisha ili upate Sifa ya kupiga Kura kuchagua Mwenyekiti wa Kitongoji, Mwenyekiti wa Kijiji na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji.
SIFA ZA KUJIANDIKISHA:
- Awe Raia wa Tanzania
- Awe na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea
- Awe na akili timamu
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa