Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro wakati wa ziara yake kushiriki shughuli za uokoaji amesema mvua zimeleta madhara makubwa ambapo watu wawili wamefariki leo hii Katika Halmashauri ya Wilaya Meru.
Dc Muro amewataja waliokufa kuwa ni Ndg. Terevaeli Mirisho Nasari Mwenye miaka 65 mkazi wa kitongoji cha meto Kijiji cha Mulala Kata ya Songoro, ambapo amefariki dunia asubuhi baada ya maporomoko ya Udongo kutoka mlimani kuvunja ukuta wa chumba alichokuwa amelala na tayari mwili wake umepatikana na kupelekwa katika Hospitali ya Mount Meru.
Pia, kifo kingine ni cha mtoto Tumaini Simon mwenye umri wa miaka 3 Mwenyeji wa kijiji cha Valeska Kitongoji cha Mwamko, ambaye amesombwa na mafuriko ya maji wakati wa harakati za kuokolewa na mzazi wake ambapo Mzee Simon alifanikiwa kuokoa mtoto mmoja tu na Mwili wa mtoto Tumaini umepatikana na taratibu za mazishi zinaendelea.
Pia Muro ameeleza kuwa nyumba 50 zimeharibiwa na zingine zimeanguka kutokana na maji kuwa mengi na tayari ameshaziagiza kamati za maafa zinazonongozwa na wakurugenzi wa Halmashauri za Meru na Arusha kushirikiana na wananchi katika kutoa misaada ya haraka katika kunusuru familia hizo ikiwemo kuwatafuta makazi ya muda,kutoa tahadhari ya wananchi waliojenga pembeni ya milima na miinuko mikubwa pamoja na wale waliojenga Katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko kuondoka katika maeneo yao haraka kabla ya madhara zaidi mana mvua bado zinaendelea kunyesha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akizundumza na wananchi wa Kijiji cha Mulala.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa