Mkakati wa Serikali kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ,VVU na UKIMWI kwa watumishi wa umma umeendelea kutekelezwa kwa kuhamasisha watumishi wote wa umma kupima afya zao jambo ambalo litawasaidia kufahamu khali zao za afya na kupata huduma stahiki.
Serikali kupitia kitengo cha ANUAI za jamii Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kinahamashisha watumishi wa umma kutumia fursa iliyotolewa ya kipindi cha mwezi mmoja na nusu kupima afya zao,akitoa hamasa hiyo Bi Anne Mazalla ambaye ni mkurugenzi wa kitengo cha ANUAI za jamii ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora amesema,namnukuu "kwa sasa hivi watumishi ni kipindi cha kupima afya zetu ambacho kimetolewa kwa mwezi mmoja na nusu hamasika kapime afya yako ukijifahamu upo katika hali gani itakusaidia wewe katika maisha yako na pia jamii nzima"
kwa kuzingatia hili watumishi wa Halmashauri ya Meru wamejitokeza kwa wingi kupima afya zao ,akithibitisha hayo Dr.W.Sango amesema akitumia uzoefu kua katika swala la upimaji wa afya changamoto kubwa kua ni hofu kwa walengwa amewapongeza watumishi hao kwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kwa lengo la kuzijua hali zao za kiafya na kuweza kupata huduma stahiki,akitoa ufafanuzi kwa watumishi walioko kwenye ngazi za kata na vijiji kua huduma hii itafanyika katika zahanati zilizopo kwa siku mbili kwa wiki na matangazo ya siku hizo yametolewa kwa Maafisa watendaji wote.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa