Wauguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru waunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi kupitia risala yao iliyo somwa mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo wakati wa maadhimisho wa siku ya Wauguzi duniani wamesisitiza "Sisi ni jeshi kubwa kati ya wahudumu wote wa afya hivyo tutaendela kutoa huduma nzuri za afya kwa wagonjwa wetu kwa weledi na kuzingatia maadili ya uuguzi".
wauguzi hao wameadhimisha siku hiyo yenye kauli mbiu "WAUGUZI NI SAUTI YA KUONGOZA, AFYA NI HAKI YA MWANADAMU" ambayo huadhimishwa Mei 12 ya kila mwaka kwa kumuenzi Bi. Florence Nightingale ambaye ndiye mwazilishi wa huduma ya uuguzi na aliweka misingi bora ya huduma ya uuguzi inayozingatia upendo, huruma, uvumilivu na ujuzi kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma hizi mchana na usiku. Siku hii huadhimishwa kila ifikapo Mei 12 ya kila mwaka.
Naye mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher J. Kazeri amewaasa watumishi wa Halmashauri hiyo kutumia vyema dhamana na rasilimali za Serikali kwa manufaa ya umma.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa