Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg.Charles Kabeho ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kuhamasisha uwekezaji katika elimu sawasawa na kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2018.
Ndg. Kabeho ametoa pongezi hizo alipoweka jiwe la ufunguzi katika Shule ya Sekondari Fransalian Hekima ambayo ni shule isiyo ya Serikali ya kidato cha kwanza hadi cha nne iliyopo kitongoji cha Kitefu katika Halmashauri hiyo.Ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo Umegharimu Shillingi 1,200,000,000.
Ndg.Kabeho amewapongeza wawekezaji hao kwa kuunga mkono jihada za Serikali katika maendeleo ya Taifa kwani ipo tayari kushirikiano na wawekezaji wanafuata sheria na taratibu.
Aidha Ndg.Kabeho amezindua klabu ya wapinga rushwa ya wanafunzi wa shule hiyo baada ya kujiridhisha na uwezo wa mapambano dhidi ya rushwa waliojengewa.
Akitoa ujumbe wa Mwenge shuleni hapo Ndg.Ipiana ambaye ni miongoni mwa wakimbiza mwenge kitaifa amesema Serikali imeboresha sekta ya elimu na kuhakikisha watoto wote haswa mtoto wa mnyonge anapata elimu bora kuanzia ngazi ya msingi hadi chuo kikuu kwa kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari pamoja na kuwawezesha wanafunzi wanaotoka familia duni kusoma vyuo vikuu kwa kuwapa mkopo ambapo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali imetenga fedha kiasi cha Bilioni 400 kwaajili ya mkopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaotoka familia zisizo na uwezo.
Ndg.Ipiana ametoa wito kwa wazazi kutimiza wajibu wao katika kuwapa elimu watoto wao ikiwa ni kuhakikisha watoto waliotimiza umri wa kwenda shule wanaandikishwa sambamba na kuwapa chakula .
Pia Ndg .Ipiana ameitaka jamii kushiriki kutimiza azma ya Serikali ya kutoa elimu bora kwa kuchangia kuboresha miundombinu ya shule .
BAADHI YA PICHA ZA TUKIO
Mbio za mwenge zilipowasili eneo la shule ya Sekondari Fransalian Hekima.
Meneja wa shule ya Fransalian Hekima Padri Tomichan P akisoma taarifa ya shule hiyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg.Charles Kabeho akishuhudia jaribio la kisayansi lililofanywa na Wanafunzi katika shule ya sekondari Fransalian , juu ya uwepo wa madini ya protini kwenye yai la kuku katika maabara ya biologia katika shule hiyo.
Matokeo ya jaribio la kisayansi juu ya uwepo wa protini katika yai la kuku lililofanywa na wanafunzi katika shule ya Fransalian mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa akikagua maabara ya kemia katika shule ya Fransalian Hekima.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Charles Kabeho akiweka jiwe la ufunguzi katika Shule ya Sekondari Fransalian Hekima.
Jiwe la ufunguzi lililowekwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa katika shule ya Sekondari Fransalian Hikima
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akizungumza baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Shule ya Sekondari Fransalian Hekima.
Ndg.Ipiana Ambaye ni Mkimbiza Mwenge wa uhuru kitaifa akitoa ujumbe wa mwenge wa uhuru katika viwanja vya shule ya Sekondari Fransalian Hekima
Wanafunzi katika shule ya Sekondari wakati mbio za mwenge wa Uhuru zilipowasili shuleni hapo.
Wanachama wa klabu ya kupinga rushwa wakisoma taarifa ya klabu hiyombele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa
picha ya pamoja kati ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa na Mkurugenzi wa shule ya Fransalian Hekima fr.Tomichan P akibeba mwenge wa uhuru ishara ya ushirikiano kati ya Serikali na wawekezaji.
picha ya pamoja kati ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa na mkuu wa shule ya Fransalian Hekima sista, Jesline Mathew akibeba mwenge wa uhuru ishara ya ushirikiano kati ya Serikali na wawekezaji.
picha ya pamoja kati ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa na Tusenambaye ni kiongozi katika shule ya Fransalian Hekima akibeba mwenge wa uhuru ishara ya ushirikiano kati ya Serikali na wawekezaji.
picha ya pamoja kati ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa na wanafunzi wa klabu ya kupinga rushwa katika shule ya Fransalian Hekima wakibeba mwenge wa uhuru ishara ya ushirikiano wa kupinga rushwa .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa