Kitengo cha TASAF kinaratibu Mpango wa kunusuru kaya maskini chini ya TASAF awamu ya III ulioanza katika Halmashauri ya Meru mwezi Julai 2014 kwa kujenga uelewa juu ya Mpango kwa wadau mbalimbali. Kaya maskini katika vijiji 47 zilitambuliwa, kuhakikiwa na kuandikishwa. Hatimaye kaya 5,800 ziliidhinishwa kupokea malipo kutoka kwenye Mpango.
Malipo kwa walengwa
Malipo kwa walengwa ambayo hufanywa kwa vipindi vya miezi miwili miwili yalianza katika kipindi cha Julai/Agosti 2015. Malipo yameshafanywa kwa vipindi 14 kuanzia Julai/Agosti 2015 hadi Septemba/Oktoba 2017 ambapo jumla ya shilingi 2,672,977,174.00 zimelipwa kwa walengwa.
Manufaa ya Malipo kwa Walengwa
Kutokana na malipo kutoka kwenye Mpango, walengwa wameweza kutekeleza shughuli mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maisha yao. Baadhi ya manufaa waliyopata ni pamoja na:
Miradi inayosaidiwa na mfuko wa OPEC III kwa mwaka wa 1
Kwa kutumia mfuko wa OPEC III, TASAF inasaidia utekelezaji wa miradi ifuatayo:
Lengo la mradi ni kutoa malazi shuleni kwa wanafunzi 48 na hivyo kupunguza tatizo la wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda na kutoka shuleni. Mradi una thamani ya shilingi 76,239,272.73 ambapo shilingi 68,637,354.00 zimetolewa na TASAF na kiasi kilichobakia ni nguvu ya wananchi wa kijiji cha Ngejusosia.
Uanzishaji wa vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa