Asilimia 64 ya wakazi wote ndani ya Halmashauri ya Meru wanapata Huduma ya Maji kutokana na vyanzo vya Chemchem, maziwa, mito, visima na uvunaji wa maji ya mvua. Hata hivyo asilimia inatarajiwa kuongezeka baada ya kukamilika kwa miradi ya Vijiji 10 inayoendelea kujengwa katika halmashauri ya meru.
Idara inaendelea na jitihada zaidi za kutafuta rasilimali zitakazowezasha ujenzi wa miradi ya maji kutekelezwa hivyo kuboresha hali ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi. Miradi hii inaweza tekelezwa kwa awamu kutegemea uwezo halisi na upatikanaji wa fedha.
Huduma ya maji safi hutolewa kwa njia zifuatazo:
Katika Halmashauri ya Meru kuna jumla ya vyombo 24 vya watumiaji maji na jumla ya Mifuko ya maji 48 ya Vijiji.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa