Halmashauri ya Wilaya ya Meru inamiliki mitambo ya kuchonga( kutengeneza) barabara ambayo ni Motor Grader na Soil Compactor(Roller) ambayo hutumika kama chanzo cha mapato.
Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Emmanueli G.Joram amesema ukodishaji huo wa mitambo ya kutengeneza barabara utaiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Meru kupata mapato ya ndani ambayo asilimia 60 ya mapato hayo itatumika kutekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma bora kwa wananchi kwani kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri hiyo kupitia Mkutano wa baraza lake imepitisha mpango wa bajeti kiasi cha Tsh 57,137,649,851.60 ikiwa Tsh. 4,000,000,000.00 zinatokana na mapato ya ndani(own source) na Tsh.53,137,649,851.60 ni fedha kutoka serikali kuu .
ili kuweza kukodisha mitambo hiyo fika ofisi za Halmashauri au wasiliana na wajumbe wa kamati ya usimamizi wa mitambo ya kutengenezea barabara inayoongozwa na mwenyekiti Shella Mduba mwenye namba ya simu 0755628387 waweza tumia barua pepe ded@merudc.go.tz karibu sana.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa