Wednesday 15th, January 2025
@BABATI - MANYARA
Hayati Baba wa Taifa , Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa Mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule ilikuwa Tanganyika). Ifikapo tarehe 14/10/2023 atakuwa anafikisha miaka 24 tangu atangulie mbele za haki huku Taifa na vizazi vyake vikiendelea na kumbukumbu ya kifo chake na kumuenzi.
Kitaifa Maadhimisho hayo huambatana na sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Makao makuu ya Mkoa wa Manyara mjini Babati Mgeni rasmi atakuwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo wa kuona mbali, hata alipopingwa baadaye waliompinga walikiri ukweli wa maono yake. Ni dhahiri kwamba Mwalimu Nyerere anakumbukwa kwa Mambo mengi ya msingi aliyoyapa kipaumbele wakati wa uongozi wake. Jambo mojawapo alilolisema Julai 29/07/1985, kwamba "kazi iliyokuwa muhimu kuliko zote kwangu Mimi , ilikuwa ni kujenga Taifa lenye umoja kwa msingi wa heshima na usawa wa Binadamu." Mwenyezi Mungu Mrehemu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa