• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Afya

 

VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA VILIVYOPO

Idara ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru in jumla ya vituo vya huduma 62 inajumuisha Hospitali 2 (1 ya serikali, 1 ya FBO) vituo vya Afya  9 (serikali 7 FBO 2) na zahanati 51( Serikali 27,FBO 13,Binafsi 9  na Taasisi 2)


GOVERNMENT
FBOs
PRIVATE
PARASTATAL
TOTAL
HOSPITAL
1
1
0
0
2
HEALTH CENTRE
7
2
0
0
9
DISPENSARIES
27
13
9
2
51
TOTAL
35
16
9
2
62

HUDUMA ZINAZOTOLEWA 

Wagonjwa wan je (OPD)

Wagonjwa wanaolazwa (IPD)

Macho

Afya za Kinywa na Meno

Huduma za mazoezi ya Viungo

Huduma za Ustawi wa jamii

Huduma za Upasuaji mdogo na Mkubwa

Huduma za Unasihi

Huduma za Maabara

Huduma za kansa

Huduma za Afya ya Mama na Mtoto

Huduma za mionzi

Duka la Dawa

MIFUMO YA MALIPO YA HUDUMA

Mifumo ya Kielektroni (E-Pay)

 Bima Msamaha kulingana na Miongozo

 

 

UJENZI WA MAJENGO YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA

 

Idara Afya ya wilaya ya Meru ina miradi 4 ya ujenzi wa majengo ambayo yametokana na uhaba wa majengo ya kutolea huduma, majengo hayo ni kama ifuatavyo:-

Jengo la huduma ya kinywa na  meno

Jengo la wodi ya mama wajawazito

Jengo la huduma ya wajawazito Zahanati ya Kwaugoro

Jengo la Zahanati ya Ambureni.

JENGO LA HUDUMA YA KINYWA NA  MENO

Ujenzi wa jengo hili ulianza tarehe 10/03/2017 baada ya makandarasi M/S BIGAN INVESTMENT SONS CO. LTD kushinda zabuni ambayo inajengwa kwa  gharama ya  Tsh73,594,900 pamoja na kodi hadi kukamilika. Jengo hili lina vyumba viwili  vya kutolea huduma ya kung’oa  meno na kurekebisha meno, na cha tatu kwa ajili ya upasuaji wa meno na mionzi. Mpaka sasa kiasi cha Tsh. 28,608,864.90 zimelipwa kwa awamu ya kwanza ambapo jengo hili lipo katika hatua ya kupauliwa. Fedha za ujenzi huu zinatokana na mapato ya duka la dawa la nje na mapato ya huduma za Hospitali. Jengo hili likikamilika linaweza kuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa mpaka 30 kwa siku.

Ambapo litanufaisha wakazi wa Meru wapatao 310,480 mara tu jengo litakapokamilika litaanza kazi kwak uwa vifaa vyote muhimu vipo.

JENGO JIPYA LINALOENDELEA KUJENGWA KWA AJILI YA AFYA YA KINYWA NA MENO

JENGO LA MAMA WAJAWAZITO.

 Ujenzi huu ulianza tarehe 02/04/2017  Kwa unafadhiliwa na shirika la “World View International “ baada ya andiko (proposal) ilioandikwa na ofisi ya Mganga Mkuu, jengo hili litakuwa na uwezo wa vitanda 30 na chumba cha upasuaji,pamoja na chumba cha watoto njiti. Mkandarasi  aliyeshinda zabuni ya ujenzi huu ni M/S BIGAN INVESTMENT SONS CO. LTD  ambaye  atajenga kwa Tsh127,947,500 pamoja na kodi  kwa awamu ya kwanza .  Hadi sasa ameshalipwa Tsh45,687,950 ambazo zitafikisha ujenzi katika hatua ya lenta pia litakapokamilika litaweza kupokea wajawazito 15 na waliojifungua  15 watoto njiti 10 na kufanya upasuaji kwa wajawazito.

ujenzi huu ni kwa awamu mbili ambapo hatua ya kwanza ipo katika hatua  ya kupaua hata hivyo ujenzi huu utakamilika kwa fedha 127,947,500/= kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili itategemea nguvu ya mfadhili ili aweze kuendelea nayo.  Jengo hili litasaidia wakazi wa Meru wapatao 310,480/=

JENGO LA MAMA WAJAWAWAZITO LINAENDELEA KUKAMILIKA ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAMA WAJAWAZITO

MIPANGO YA BAADAYE

Kuendelea kufanya mawasiliano na mfadhili ili aweze kuruhusu fedha za awamu ya pili ya kuongezea jengo hilo

JENGO LA HUDUMA YA WAJAWAZITO ZAHANATI YA KWAUGORO

Jengo hili lilianza kujengwa tarehe 10/04/2016 kwa ufadhili wa “Lions club Tilburg na Wilde Genzen” ulisimamiwa na Adra Tanzania ambapo limegharimu Tsh. 93,00.,000/=likiwa na vyumba 3, chumba cha kusubiria, kujifungulia, pia kina ofisi 2, vyoo 2 vya ndani na bafu 2, jengo hili litaweza kuwekwa vitanda 12 na vya kujifungulia 3  katika jengo hili kunahitajika vitanda 12, kujifungulia 3 na samani kwa ajili ya kutolea huduma.

Jengo kamilika

Mradi huu utasaidia wakazi wapato 2,590 wa kijiji cha kwa Ugoro chenye kaya 558.

Changamoto

Kuna uhitaji wa vitanda vya kusubiria kujifungulia vipatavyo 12

Vitanda vya kujifungulia 3

Na kuna uhaba wa samani katika jengo hilo

Wanufaika 

Wakazi 2,590 wa kijiji cha kwa Ugoro ndiyo watakaofaidika na mradi huo, kwani utapunguza safari ndefu kwenda katika huduma ya kujifungua

Mpango wa baadaye

Tunaendelea kuwasiliana na mfadhili ili waweze kutununulia samani na vitanda hivyo

JENGO LA ZAHANATI YA AMBURENI

Kata ya Ambureni ina wakazi 8,799 ambao walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya. Wananchi kwa kushirikiana na WAMATA wamejenga Zahanati ili kuwapunguzia wananchi adha ya kufuata huduma ya Afya. Jengo hili lilianza tarehe 14/04/2016 ambapo limegharimu jumla ya Sh. 57,000,000/= zikiwepo nguvu za wananchi ambapo wananchi wamechangia kununua kiwanja hicho chenye thamani ya 19,000,000/= (hata hivyo ili Zahanati hii ianze kufanya kazi inahitajika samani vifaa  vya kitaalmu na madawa.

JENGO LA UTAWALA

JENGO LA UTAWALA LINALOENDELEA KUJENGWA KWA AJILI YA TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA ZA AFYA(CHMT)

MIRADI YA IDARA YA AFAYA

Idara ya Afya ina mradi wa duka la dawa kama chanzo cha kuimarisha huduma na kutatua changamoto ya upungufu wa dawa kwa wagonjwa wanaokosa dawa ndani ya hospitali.

 

Mradi wa duka la dawa la idara ya Afya unafahamika kwa jina Meru Pharmacy.

 

CHANGAMOTO

 

Changamoto za vitendea kazi

 

Kutokua na chumba cha kuhifadhia miili (mortuary)

   

Mipango ya Baadaye

 

Kupelekea vifaa vya tiba vya kuanzia kazi

 

Kuendelea kuwasiliana na wafadhili  na wadau mbali mbali katika kutekeleza majukumu ya idara

 

WADAU WA IDARA YA AFYA MERU DC

 

DSW

 

EGPAF

 

ENGENDER HEALTH

 

JHIPIEGO

 

PATH

 

STEMM

 

MARIE STOPES

 

WORLD VISION

 

WHO

 

NHIF

 

KNCV

 

PSI

 

REDCROSS

   

Ni matumaini yetu kwamba juhudi mbalimbali tunazoendela kuchukua zitasaidia kupunguza uhaba ya miundo mbinu ya kutolea huduma za afya.

        

AFYA TIBA

 

Idara inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na kutekeleza mpango mkakati wa afya wa mwaka 2015 -2020. Katika kuhakikisha wananchi wanapata tiba sahihi,

 

Majukumu yafuatayo:

 
  • Kusimamia manunuzi ya dawa, vitendanishi vya maaabara ,vifaa na vifaa tiba kisha kuvisambaza kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
  • Kutoa huduma za matibabu na uuguzi kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya zikiwemo huduma za upasuaji mkubwa na mdogo. Huduma hizi ni kwa wagonjwa wa nje na wagonjwa wa kulazwa.
  • Kufanya ukaguzi wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
  • Kusajili na kuhuisha maduka ya dawa na vipodozi, kuyafanyia ukaguzi mara kwa mara na kuhakikisha yanafuata sheria, kanuni na miongozo inayosimamia uanzishaji na uwepo wa maduka hayo
  • Kusimamia pamoja na kuzikagua maabara zote na kuhakikisha zimesajiliwa na zinatoa huduma bora kulingana na miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya.
  • Kutoa, kusimamia na kuratibu huduma za afya ya uzazi na mtoto katika Manispaa . Huduma hizi ni pamoja na uzazi salama, huduma za uzazi wa mpango, huduma za chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito, uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti. Huduma nyinginezo ni pamoja na huduma za kuzuia ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.
  • Kuratibu huduma za kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na UKIMWI. Huduma zitolewazo ni pamoja na matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, huduma za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto, huduma za kuchunguza na kutibu magonjwa ya ngono pamoja na huduma za wagonjwa majumbani. Huduma hizi hutolewa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
  • Idara inashughulikia pia masuala ya ustawi wa jamii ambapo inahakikisha makundi maalumu yanaatambuliwa na kuunganishwa na mpango wa matibabu bila maalipo. Makundi haya ni pamoja na wazee, walemavu na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
  

AFYA KINGA

 

Idara imeendelea kutekeleza majukumu mbalimbali yanayolenga kuwakinga wananchi na magonjwa ya kuambukiza. Mojukumu hayo ni pamoja na:

 
  • Ukaguzi wa nyumba za kuishi na majengo ya biashara kama vile nyumba za kulala wageni,majengo ya kutengeneza na kuuza vyakula ili kuondoa machukizo yanayoweza kuhatarisha afya ya binadamu.
  • Utoaji wa elimu ya afya kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya afya.
  • Utoaji wa chanjo kwa magonjwa ya kuambukiza kwa wajawazito na watoto
  • Usimamizi wa afya na usalama mahala pa kazi
  • Usimamizi wa usafi wa Mazingira.
  

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa