Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Kimeanzishwa mwaka 2012 kulingana na muundo mpya wa serikali za mitaa. Kabla ya kuwepo kwa kitengo hiki majukumu yanayohusiana na kitengo hiki katika Halmashauri ya Meru yalikuwa yakiendelea kutekelezwa kwani wataalamu wa fani hiyo tayari walikuwepo.
Halmashauri ya Meru ni moja kati ya Halmashauri ambazo zina Mtambo (Server) wa kusambaza mtandao katika kila ofisi, hivyo kupunguza usumbufu wa watumishi kutoka nje ya ofisi kwa ajili ya kutuma taarifa zao.
Kitengo kwa Kushirikiana na menejimenti kimeandaa Sera ya TEHAMA (ICT POLICY) Kwa lengo la kusimamia na kutekeleza masuala yahusuyo TEHAMA katika Halmashauri ya Meru.
Vile vile Halmashauri kupitia kitengo cha TEHAMA inaendelea kutekeleza MWONGOZO WA MATUMIZI BORA, SAHIHI, NA SALAMA YA VIFAA NA MIFUMO YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA) SERIKALINI wa mwaka 2012
MAJUKUMU YA KITENGO
Kitengo cha TEHAMA kinatekeleza majukumu yafuatayo ikiwa ni pamoja na mengine kulingana na maelekezo ya Mkurugenzi
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa