Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Jeremia Kishili amewataka Watendaji wa Kata kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi inayotekelezwa kwenye kata zao.
Pia, Mhe. Kishili amesisitiza Watendaji wa Kata kuwasilisha taarifa za lishe kutoka kwenye Kata zao kama ambavyo wanawasilisha taarifa nyingine zinazotekelezwa katika Kata ili kujua hali ya lishe katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Amesema hayo, leo katika Mkutano wa Baraza la Halmashauri siku ya kwanza, kujadili taarifa za Kata kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa