Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda amefanya ziara na kukagua Soko la Tengeru lililopo Kata ya Akheri, Halmshauri ya Wilaya na Meru na kufanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo na kusikiliza changamoto wanazozipitia katika shughuli zao na kuahidi kuzitatua kwa kufanya maboresho.
Moja ya changamoto iliyowasilishwa na wafanyabiashara kwa Mhe. Kaganda ni pamoja na uharibifu wa miundombinu hasa katika kipindi cha mvua inayosababisha hali ya soko isiwe rafiki na kushindwa kufanya biashara zao kwa amani.
Mhe. Kaganda ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Divisheni ya Biashara hukakikisha maeneo yote yaliyoharibiwa na mvua yanajazwa mchanga. Vilevile, Kaganda amemwelekeza Mwenyekiti wa Soko hilo kuhakikisha anasimamia zoezi la kuwapanga wafanyabiashara wa aina moja kukaa sehemu moja ili kuleta mpangilio mzuri wa soko.
Hata hivyo, Mhe. Kaganda amewataka wataalamu wa Divisheni ya miundombinu kuandaa Mpangilio wa Soko kwa njia ya ramani (layout) utakayosaidia kuonesha soko lilivyo. Sambamba na hayo, Kaganda amesisitiza Maafisa Afya kuhakikisha wanatoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusiana na kuzingatia usafi na utunzaji wa mazingira katika soko hilo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa