Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mohamed Mkalipa leo tarehe 24 Oktoba, 2024 amekutana na mashirika yasiyo ya kiserikali NGO's zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa lengo la kufahamiana na kutoa maelekezo mbalimbali kulingana na kazi wanazozifanya.
Mhe. Mkalipa ameyataka mashirika hayo kutimiza wajibu wao wa kisheria ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa za kila robo mwaka na kuonyesha kazi zinazoendelea katika mashirika hayo. Pia ameyataka mashirika ambayo hayajasaliji makao ya watoto kufanya hivyo ndani ya siku 30 toka kikao hicho kufanyika.
"Kikao chetu cha leo ni kwa lengo la kukumbushana kutimiza wajibu wetu sisi kama Serikali na nyinyi kama mashirika kutimiza wajibu wenu lakini kuishauri Serikali na kutengeneza mikakati ya kuboresha NGO's zilizopo Meru". Amesema Mkalipa
Rabieth Kajiru ni Mshiriki kutoka Shirika lisilo la kiserikali BOSASELI ametoa shukrani kwa Mhe. Mkuu wa Wilaya na kwa niaba ya NGO's zilizoshiriki amemuhakikishia kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa za kila robo. Wamefurahi Mhe. Mkalipa kuwaandalia siku maalumu ya kujadili changamoto zao ili kuweza kuleta maendeleo .
Afisa Maendeleo ya Jamii na Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Japhet Kazeri ameeleza kuwa mbali na kuwa na mashirika 136 katika Halmashauri ya Meru Mashirikia 51 tu ndiyo yapo Hai na yanayotoa huduma hivyo kikao hichi kitatoa mwanga kwa Halmashauri kuweza kujua uhai wa mashirika yote na kazi wanazofanya.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa