Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wamefanya ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru wa kiasi cha shilingi Milioni 320,000,000.00
Kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti Mhe. Jeremia kishili wamekagua ujenzi wa nyumba tatu ambazo zinajengwa katika eneo la Zulfiroz Kiwawa.
Mradi huo ambao unasimamiwa na timu ya menejimenti ikiongozwa na Mkuu wa Idara ya Miundombinu na Maendeleo Mijini na Vijijini Mhandisi Asnath Marero ameeleza kuwa hadi sasa nyumba moja ipo hatua ya umaliziaji ikiwa imeshawekwa mfumo wa umeme na maji kwa awamu ya kwanza na kupigwa plasta. Aidha, nyumba ya pili ipo hatua ya kufunga lenta na nyumba ya tatu ipo hatua ya kumimina Zege ya lenta na kazi zinaendelea.
Wajumbe wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kupatikana kwa fedha za mradi huo.
Ukaguzi huo ni utaratibu wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa