Halmashauri ya Wilaya ya Meru imepokea zaidi ya shilingi Milioni 482 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na Matundu ya Vyoo katika shule za Sekondari 8 Katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Shule hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari Muungano, Akheri, Kitefu, Nasholi, Kiwawa, Imbaseni, Meru na Kikwe.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango Katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru wamefanya ukaguzi katika shule ya Sekondari ya Muungano Usariver iliyopo Kata ya Usariver, ambapo kati ya fedha zilizopokelewa kutoka Serikali kuu shule hiyo imepokea kiasi cha shilingi Milioni 114,400,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne na matundu ya 8 ya Vyoo katika shule hiyo.
Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Jeremia Kishiri wamekagua ujenzi wa madarasa manne ambayo yapo katika hatua ya kusimamisha Mbao za kupaua.
Pia, Wajumbe hao wametembelea mradi wa choo ambao unaendelea kutekelezwa.
Ukaguzi huo ni utaratibu wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne na ya mwisho kwa mwaka wa Fedha wa Serikali wa 2023/2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa