Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul C. Makonda ametoa muelekeo wa kufanya kazi katika Mkoa wa Arusha na kueleza kuwa atafanya kazi kwa kusimamia haki na kuhakikisha hakuna mwananchi anazurumiwa haki yake katika Mkoa huo.
Mhe. Makonda ameeleza hayo leo katika hafla ya makabidhiano yaliyofanyika kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ndg. John V.K Mongella ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu CCM Taifa Bara katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi wote na watendaji kuhakikisha wanawajibika kwa nafasi zao ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Makonda pia, amesisitiza maelekezo aliyopokea kutoka kwa Mhe.Rais Dkt. Samia kuhusu suala la kuimarisha Utalii katika Mkoa wa Arusha, pia ameeleza kuwa Serikali ya Dkt. Samia imeridhia mpango wa kujenga kumbi kubwa za mikutano ambayo inauwezo wa kubeba watu elfu5 na watu elfu 10.
Hata hivyo, ametoa maelekezo kwa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa kuhakikisha Pasipoti za kusafiria zinatolewa ndani ya siku 7 badala ya siku 14 kama ilivyokuwa awali.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa