Mchezaji wa Kimataifa wa Morocco katika kablu ya PSG ya Ufaransa Achraf Hakimi ameeleza kuwa amefurahi sana kwa mara ya kwanza kutoka na kutoa msaada nje ya Morocco.
Aidha, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha jambo hili linafanikiwa na kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum ili kuwezesha watoto hawa kufikia ndoto zao.
Vilevile, Achraf Hakimi ameahidi kuendelea kutoa msaada katika shule ya Sekondari ya Patandi na kutengeneza historia ya pamoja watoto hao.
rais wa Klabu ya Yanga Hersi Said ameeleza kuwa, mchezaji Achraf Hakimi
alipotaka kuja mapumziko yake Nchini Tanzania aliona ni vema asiishie kufanya utalii na kuondoka bali atoe msaada kwa watoto wenye uhitaji maalumu na Shule ya Sekondari Patandi maalumu ilipendekezwa iwe shule ya kwanza kupata msaada huo.
rais Hersi amesema, msaada wa vitu vilivyotolewa ni pamoja na kununua kompyuta 50, Laptop 5 za walimu, Vifaa Maalumu vya kusomea wanafunzi wenye uoni hafifu, Photocopy mashine, Projectors kwa ajili ya kuwasaidia walimu kuandaa vipindi kwa wanafunzi wasiweza kusikia ili kujifunza kwa kuona, Boila ya Maji pamoja na ujenzi wa kichomea taka .
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hassan Abbas Said kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Maliasili na Serikali, ametoa shukrani kwa Achraf Hakimi kwa msaada aliotoa kwa shule ya Sekondari Patandi Maalum.
Mhe. Abbas amemkaribisha Achraf Hakimi kutembelea vivutio vingine vya utalii vilivyopo Nchini Tanzania kwani maeneo aliyotembelea ni sehemu tu lakini Tanzania ina utajiri wa vivutio vingi ambavyo angependa avione na siyo rahisi kutembelea vivutio hivyo kwa mara moja.
Pia, ameeleza kuwa jambo alilolifanya ni mfano wa kuigwa kwani wapo watu mbalimbali wanakuja lakini yeye ameona asiishie kufanya utalii bali kusaidia watoto wenye uhitaji maalum.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa