Shirika lisilo la Kiserikali la SOS linalotoa huduma kwa Watoto, Vijana na Familia limetoa ufadhili wa Masanduku 22 ya Maoni ambayo yatafungwa katika shule za Sekondari na Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mwakilishi wa Shirika la SOS Porches Masawe amekabidhi masanduku hayo leo Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo Halmashauri itasambaza katika shule za Sekondari na Msingi ambazo zina Miradi ya BOOST na SEQUIP lakini pia kwa Shule zilizoundwa Mabaraza ya Watoto.
Afisa Maendeleo ya Jamii Florah Msilu ameeleza kuwa masanduku haya yatasaidia sana watoto kutoa maoni yao dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa shuleni, nyumbani na hata mtaani ili kuweza kupata msaada.
Aidha, Msilu ametoa shukrani kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mwl. Zainabu J. Makwinya kwa Shirika la SOS kwa ufadhili wa Masanduku hayo.
Ikumbukwe kwamba huu ni utekelezaji wa mpango wa Shule Salama uliojikita katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kupunguza vikwazo vya upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi wote.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa